Ala za sauti za lugha ikiwemo sifa bainifu katika lugha ya binadamu

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Wednesday, December 5  2018 at  09:57

Kwa Muhtasari

  • Baadhi ya wadau wa Kiswahili wanasema chemba ya huku wengine wakirejelea vijishimo vya ala za sauti kama chemba cha
  • Hili liwe suala la siku nyingine

 

KATIKA makala iliyopita, tuliangazia viungo mbalimbali vinavyofahamika kama alasauti katika fonetiki.

Hii leo tutaendeleza mada hii kwa kuchambua ala sauti zilizosalia jinsi ifuatavyo:

 

Ulimi

Hii ni ala muhimu sana katika matamshi, huweza kujongea sehemu mbalimbali za chemba ya kinywa. Ulimi umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni ncha ya ulimi, bapa la ulimi na shina la ulimi.

Meno

Meno ya juu na ya chini, husaidia katika utoaji wa sauti za meno pale yanapokutana au kugusana na ncha ya ulimi au midomo.

 

Midomo

Midomo ni muhimu sana katika uzalishaji wa sauti za lugha.Midomo inapokutana huzalisha sauti kama [p] na [b] au [m]

 

Epigloti

Hiki ni kipande cha msuli kinachotenganisha njia ya hewa na njia ya chakula.

 

Chemba cha Pua

Wakati kilimi au kaa kaa laini likiteremka huruhusuhewa kupita katika mkondo wa hewa wa kinywani. Vilevile wakati huohuo hewa hutatizwa na ala mbali mbali za sauti kinywani, husababisha kutolewa kwa sauti za pua kama [m], [n] na [ɲ].

Chemba cha Kinywa

Hii ni sehemu inayohusisha alasauti nyingi zaidi kuliko chemba yoyote katika utamkaji wa sauti. Sauti za kinywa hupatikana pale kaakaa laini inapopanda na kuziba hewa isipite katika chemba cha pua.

Sauti nyingi huzalishwa katika chemba cha kinywa.

 

UBAINISHAJI WA SAUTI ZINAZOTUMIKA KATIKA LUGHA YA MWANADAMU

Mchakato mzima unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya alasauti huishia kuzalisha sauti za lugha au ukipenda vitamkwa vya lugha au foni.

Kazi kuu ya mwanafonetiki ni kuchunguza michakato yote ya uzalishaji lugha, kujifunza na  kubainisha sauti mbalimbali za lugha na kisha kuziainisha kwa kuzipa sifa maalumu zinazofahamika kama sifa bainifu.

Jinsi tulivyotaja awali sauti za lugha zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni:

i. Konsonanti 

ii. Irabu au vokali

 

Konsonanti

Hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati hewa inayopita katika mkondo wa hewa kutokea mapafuni inatatizwa au kuzuiliwa na ala mbalimbali za sauti.

 

 

Marejeo:

Massamba, D.P.B. (2002). Historia ya Kiswahili 50 BK. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ipara, I. O., Waititu, F.G., (2006) Ijaribu na Uikarabati, Nairobi: Oxford University Presss.

Habwe, J., (2006). Darubini ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers