Dhana ya Semantiki ya Kiswahili

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Wednesday, September 27  2017 at  06:15

Kwa Mukhtasari

Semantiki ni maana katika ngazi ya sentensi.

 

KWA muhtasari semantiki ni maana katika ngazi ya Sentensi.

Katika mada hii tutajadili na kuchambua vipengele vinavyohusu maana katika ngazi ya sentensi au tungo.

Mojawapo wa mambo yanayoibua maana katika ngazi ya sentensi ni kanuni ya ufungamanifu.

KANUNI YA UFUNGAMANIFU

Kwa mujibu wa kanuni ya ufungamanifu maana ya kiambo changamani cha kisintaksia (kirai, sentensi) inatokana na maana ya viambajengo vya kiambo hicho na mahusiano ya kisarufi.

Uhusiano wa kanuni hiyo unadhihirika pale ambapo maneno yale yale yanatumika kuunda sentensi zenye maana tofauti kutokana na tofauti za uhusiano wa kisarufi. Kwa mfano:

  1. Nyani alimkimbiza mtoto
  2. Mtoto alimkimbiza nyani
  3. Jangili amemuua nyani
  4. Nyani amemuua jangili

Hata hivyo kanuni ya ufungamanifu haifanyi kazi sana katika nahau. Hii ni kwa sababu nahau ni mafungu ya maneno ambayo maana zake mara nyingi hazitokani na muunganiko wa maana wa maneno yanayoziunda hizo nahau. Nahau si fungamanifu na mpangilio wake ni muhimu na hauwezi kubadilishwa.

kwa mfano:

i. kuvunja ungo,

ii. kuzunguka mbuyu

iii. kuvaa miwani.

Mifano hii ina maana ya moja kwa moja ukivuruga unatoa maana yake. Nahau zina tabia ya maneno (yaani kuwa kama maneno) na kwa sababu hii huchukuliwa kama leksimu moja na maana yake itachunguzwa kama neno moja.)

SIFA NA UHUSIANO WA MAANA KATIKA NGAZI YA SENTENSI/TUNGO

Tutachambua na kuchambua sifa hizi katika vipengele vifuatavyo:

1. USAWE

Ni uhusiano wa kimaana baina ya sentensi mbili au zaidi ambapo sentensi hizo huwa na maana moja ya msingi. Kwa mfano

'nilikutana na ajuza njiani' na 'nilikutana na bikizee barabarani‘

Aina za Usawe

Kuna aina kadhaa za usawe kama tutakavyoziainisha hapa:

i. Usawe wa Kileksia

Huu ni usawe unaotokana na sentensi mbili au zaidi kuwa na maneno yenye maana ile ile ya msingi katika nafasi ile ile.

Kwa mfano:

'Sikujua kuwa usingeongea naye Abadan au 'Sikufahamu kama usingezungumza naye asilani'

Uhusiano kati ya sentensi hizo ni uhusiano wa kisinonimia.

ii. Usawe wa Kimuudo

Hii hujitokeza pale ambapo maana ya msingi ya sentensi mbili au zaidi kubaki ile ile ingawa sentensi hizo zina mpangilio tofauti.

Usawe huu ni wa kimuundo kwa sababu haugongani na usawe wa maneno yaliyotumika. Kwa mifano:

Maelezo yake yalikuwa magumu kueleweka‘ na ilikuwa vigumu kuelewa maelezo yake

2. UTATA

Ni hali ambapo sentensi moja huwa na maana zaidi ya moja au huweza kueleweka kwa namna zaidi ya moja.

Aina za Utata

i. Utata wa Kileksika

Huu ni utata ambao husababishwa na neno au maneno fulani yaliyotumika katika sentensi ambayo yana maana zaidi ya moja. Kwa kawaida utata wa kileksika hutokana na matumizi ya uhonimia na upolisemia. Kwa mfano:

a) Baada ya shida nyingi alifanikiwa kumleta Papa nyumbani

1. Samaki

2. papa wa kanisa katoliki

ii. Utata wa kimuundo

Huu hutokana na jinsi sentensi zilivyopangiliwa na kutokana na umbo/neno/kirai kuwa katika nafasi maalumu katika sentensi. Kwa mfano:-

Wanaume na wanawake waangalifu walikaa kando.

maana zake: