Fasihi Bunilizi ya Kisayansi na Fasihi Bunilizi ya Kinjozi au Fantasia

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, November 13  2018 at  15:42

Kwa Muhtasari

Fasihi andishi bunilizi uinaweza kuwa ni ya kisayansi au ya kinjozi

 

JINSI tulivyotaja katika makala ya awali fasihi andishi bunilizi inaweza kuainishwa katika matawi mawili jinsi ifuatavyo:

  1. Bunilizi ya kisayansi
  2. Bunilizi ya kinjozi

 

Fasihi andishi Bunilizi ya Kisayansi

Ni utanzu wa fasihi andishi bunilizi ambapo mwandishi hujikita katika mambo ya ya kiteknolojia na sayansi. Mwandishi husifu mambo ya teknolojia na fasihi ikiwemo maendeleo na hatua katika ulingo wa sayansi na teknolojia.

Sanaa hii inaweza kuonyeshwa katika filamu za kisayansi, vitabu na majarida anuai ya masuala ya kisayansi ya teknolojia.

Kwa mfano Alien vs Predator ya Paul W.S. Anderson ni filamu ya bunilizi ya kisayansi (2004) inayoonyesha kuwepo uhai katika sayari nyinginezo.

 

Bunilizi ya kinjozi au bunilizi ya kifantasia

Ni utanzu wa fasihi andishi bunilizi ambapo mwandishi hutumia matukio, mandhari na wahusika wasio wa kawaida.

Baadhi ya mifano ya kazi za bunilizi ya kijonzi ya Kiingereza ni kama vile:

"The Lord of the Rings” - (Bwana wa Pete) ya J.R.R Tolkien

"Gulliver's Travels” – Safari za Guliver ya Jonathan Swift

"A Midsummer Night's Dream” – Ndoto ya Usiku mmoja wa Majira ya Kiangazi ya William Shakespeare.

Tofauti kati ya Bunilizi ya Kinjozi na Bunilizi ya Sayansi

Bunilizi ya kinjozi hutofautiana na bunilizi ya kisayansi kwa msingu huu: Kinyume na bunilizi ya kisayansi inayosifu matukio ya kisayansi na kiteknolojia, bunilizi ya kinjozi hujikita katika visa vya kiajabu visivyo vya kawaida na viumbe vya visa asili katika kuelezea matukio asilia mathalan kiini cha watu kufariki duniani na kadhalika.

 

Fasihi Andishi Ukweli

Dhana ya kweli inaashiria lengo la akili katika kujua mambo yote kwa dhati kadri inavyowezekana.

Ukweli ni dhana ya kidhahania inayoweza kujulikana kuanzia kwa hisia, fikra lakini pia kwa kufuata imani ya dini fulani inayoaminika chanzo chake ni Mungu.

Dhana au wazo hili ni la msingi hasa katika Ukristo na inasawiriwa kwa namna ya pekee katika Injili ya Yohane.

Japo fasihi andishi ina tanzu mbalimbali, inasheheni sifa bainifu zinazoitofautisha na fasihi simulizi.

Marejeo:

Falkenstein, A. 1965 Zu den Tafeln aus Tartaria. Germania 43, 269–273

Maxim, Z. 1997 Neo-eneoliticul din Transilvania. Bibliotheca Musei Napocensis 19. Cluj-Napoca

Paul, I. 1995 Vorgeschichtliche untersuchungen in Siebenburgen. Alba Iulia

Vlassa, N. 1965 --- (Atti UISPP, Roma 1965), 267–269