habari

ICC: Kamati itekeleze haki

Na Fredy Azzah na Boniface Meena  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Thursday, October 30  2008  at 14:13

WAKENYA wanaposubiri uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuhusu washukiwa sita wa ghasia zilizofuata uchaguzi mkuu wa 2007, kumekuwa na kila aina ya matamshi na harakati.
Kuna habari kuwa Serikali imebuni kamati ya Baraza la Mawaziri kuangazia kwa kina iwapo Bw Uhuru Kenyatta na Bw William Ruto wanastahili kuwania urais, mashtaka dhidi yao yakithibitishwa.
Hatua hii ni nzuri kwa kuwa Mkuu wa Sheria Prof Githu Muigai atapata fursa ya kujadiliana na wanasiasa ambao wengi ni mawakili kuhusu jambo hilo muhimu. Kisha wataamua kama Sura ya Sita ya Katiba au Sheria kuhusu Maadili ya Watumishi wa Umma, zitawaruhusu Bw Kenyatta na Bw Ruto kuwania viti vya kuongoza nchi.
Hata hivyo, wasiwasi wetu ni kuhusiana na uanachama wa wanakamati wawili, ambao wameshatangaza kuwania urais.
Profesa George Saitoti ambaye ni mwenyekiti wa kamati na Waziri wa Mashauri ya Kigeni Bw Moses Wetangula, wanatarajiwa kuwania wadhifa huo wa juu zaidi nchini.
Iwapo muungano wa PNU Alliance utataka kuteua mgombeaji mmoja, basi Prof Saitoti huenda akaonekana kuwa mtu asiyefaa kuamua hatima ya Bw Kenyatta na Bw Ruto.
Yeye atawania mchujo sawa na wanasiasa hao wawili. Itakuwa vigumu sana kuamua kuwa wanapaswa kuwania urais, akijua ni wapinzani wake.
Ni matumaini yetu kwamba Prof Saitoti atatekeleza jukumu lake la uenyekiti bila kuegemea upande wowote.
Iwapo Bw Kenyatta na Bw Ruto watathibitishwa kuwa na kesi, uamuzi wa kama wanafaa kuwania urais au la unafaa kuwa wa Mahakama Kuu au Tume nyingine husika.
Tume ya Usimamizi wa Haki inayoongozwa na Bw Otiende Amolo na ile ya Utekelezaji Katiba (CIC) ya Bw Charles Nyachae, zafaa kupewa nafasi ya kutoa rai zao kwanza.

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel