Tezi dume inatibika kwa dawa za asili

Imepakiwa - Friday, May 17  2019 at  12:50

 

Kisarawe. Ili kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, wanafunzi wa Shule ya Msingi Palaka wamefundishwa kunawa mikono kila watokapo maliwatoni.

Mwalimu wa afya shuleni hapo, Husna Mohamed anasema mafunzo hayo yametolewa kupitia klabu ya afya waliyonayo.

“Baada ya mafunzo haya, wanachama wa klabu huwafundisha wenzao unawaji wa mikono kila watokapo kujisaidia,” amesema Husna.

Husna amesema hayo wakati wa makabidhiano ya vyoo vya wasichana vilivyojengwa shuleni hapo na Shirika la Plan International. Amesema watoto wengi huugua magonjwa ya matumbo kwa kutojua kunawa vizuri.

Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo, Gwyneth Wong amesema wanachofanya ni kuwajengea uwezo wanafunzi kufikia ndoto zao kielimu ndio maana wamesaidia ujenzi wa choo hicho kuhakikisha wanaimarisha afya ya wasichana wakiwa shuleni.

Mwenyekiti wa klabu hiyo ya afya, Mariam Habib amesema “mimi na wenzangu huwa tunawasaidia wanafunzi wa darasa na kwanza na la pili kunawa mikono.”