http://www.swahilihub.com/image/view/-/3174194/medRes/1310731/-/sq5p4t/-/blakauti.jpg

 

‘Dada poa’ wa Kiwengwa wamtibua DC

Nguvu za umeme kupotea

Eneo zima la mji pamoja na viunga vyake usiku nguvu za umeme zikiwa zimepotea. Picha/HISANI 

Na MUHAMMED KHAMIS, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  13:15

Kwa Muhtasari

Siku hizi jamii imepotoka kiasi cha kuonekana kushabikia tabia za ukahaba.

 

VISIWANI ZANZIBAR

BAADA ya kushamiri kwa biashara ya ukahaba ‘dada poa’ katika shehia ya Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, mkuu wa wilaya ya Kaskazini B Unguja, Rajab Ali Rajab ameitaka jamii kushirikiana ili kukomesha biashara hiyo.

Amesema wakati alipochaguliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo aliikuta shehia ya Kiwengwa ikiwa na uchafu wa kupindukia kupitia biashara ya ‘dada poa’ ambayo ilishaanza kuzoeleka na kuonekana kama ya kawaida.

“Kulikuwa na hadi vibanda maalumu vya kufanyia kazi hiyo na watu walikuwa wanatoka mjini kufuata huduma hiyo. Kibaya zaidi ni kwamba wengine walikuwa na umri mdogo sana – kati ya umri wa miaka 15 hadi 20,’’ alisema Rajab.

Rajab alisema operesheni maalumu ya safisha Kiwengwa kwa asilimia 95 imefanikiwa kwani hivi sasa biashara hiyo imepungua na inafanyika kwa kificho tofauti na hapo awali na kwamba anaamini itamalizika kabisa.

Alisema operesheni hiyo inafanywa na watendaji wa wilaya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na kwamba wakati wanaianza ilikuwa ni kawaida kwa wiki kukamata watu hadi 190 wenye kujihusisha na matendo hayo.

Akizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa jumuiya inayojihusisha na changamoto zinazowakabili vijana visiwani hapa (Zafayco), Abdallah Abeid aliwaasa kutojihusisha na tabia hiyo ili kuziweka salama afya zao.

Alisema haipendezi kuona vijana wadogo wanajiingiza kwenye biashara hatari ya ukahaba.