Nape ajiuzulu kamati ya Bunge

Nape Nnauye 

Imepakiwa - Thursday, February 7  2019 at  12:36

Kwa Muhtasari

Nape Nnauye ametangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Nape, ambaye ni Mbunge wa Mtama (CCM) alijiuzulu jana jioni wakati kamati aliyokuwa anaiongoza inawasilisha taarifa yake ya mwaka 2018 bungeni jijini Dodoma leo.

 

 

Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Nape Nnauye ametangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Nape, ambaye ni Mbunge wa Mtama (CCM) alijiuzulu jana jioni wakati kamati aliyokuwa anaiongoza inawasilisha taarifa yake ya mwaka 2018 bungeni jijini Dodoma leo.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alithibitisha taarifa hiyo jana usiku alipozungumza na Mwananchi kwa simu kutoka mjini Dodoma. “Ni kweli na mimi barua nimeiona.”

Mwananchi lilipotaka kujua sababu za Nape kujiuzulu, Kagaigai alisema, “anataka ku-concetrate kwenye ubunge wake.”

Nape, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekuwa mwenyekiti wa pili kujiuzulu nafasi hiyo akitanguliwa mwaka jana na Hawa Ghasia aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti.

Ghasia na Nape ambao ni wabunge kutoka mikoa ya Kusini wanakumbukwa jinsi walivyolitikisa Bunge kutokana na sakata la korosho mwaka jana jambo ambalo lilifanya Serikali kuingilia kati na kwenda kununua korosho kwa wakulima, mchakato ambao unaendelea mpaka sasa..