Wabunge wamtoa jasho May

Theresa May. Waziri mkuu 

Imepakiwa - Friday, March 15  2019 at  14:03

 

London. Wakati wabunge wa Uingereza jana wakipiga kura tena, awali walipinga hatua ya kuondoka katika Umoja wa Ulaya bila makubaliano.

Serikali jana imewasilisha muswada unaopendekeza kuongezwa kwa muda wa kuondoka kutoka Machi 29 hadi Juni 30 iwapo wabunge wataidhinisha makubaliano yaliyoafikiwa na Waziri Mkuu Theresa May.

Makubaliano hayo yamekataliwa mara mbili na May ameonya iwapo hayataidhiniswa hali inaweza kuwa mbaya.