Biashara haramu

Na Na Ackley Ludovick

Imepakiwa - Tuesday, March 5  2019 at  16:30

 

Diana yuko ndani ya ofisi yake nadhifu sana akipitia taarifa mbalimbali za kikazi.  Ghafla simu yake ikaita na alipoipokea akafahamishwa kuwa kuna mgeni muhimu anataka kumwona. Mgeni mwenyewe alipomuona  kuanzia hapo wakawa pamoja kama chanda na pete. 

Je, ni nani huyo? Endelea.

Ilikuwa ni ofisi kubwa yenye meza moja kubwa, viti vikubwa viwili kwa ajili ya wageni wawapo ofisini hapo. Meza ilijaa mafaili yaliyokuwa na nyaraka muhimu za kampuni ya THE GREAT DIANA. Ilikuwa ni kampuni iliyojihusisha na uagizaji na  usambazaji wa samani. Nyuma ya meza alikaa mwanamama aliyekuwa na mvuto sana. Aliitwa Diana Mavune Mutozya. Kampuni hii ya uuzaji na usambazaji wa samani ilikuwa ni mali yake. Wakati akipitia baadhi ya mambo muhimu  kwa maslahi ya kampuni alisikia mlio wa simu yake ya mezani.  Hakuwa na tabia ya kupuuzia simu. Akainua na kuiweka sikioni.

“Hallow! Nani? Mruhusu aingie.” Akarudisha  mkono wa simu na kuendelea na kazi.

Hakupita muda mrefu akaingia kijana mmoja mtanashati. Alikuwa amevalia suti ya rangi ya bluu. Alionekana kama mtu mwenye uwezo kimaisha.

“Karibu!” Diana akamkaribisha.

“Shukrani!” Kijana akakaa kwenye kiti na kusalimiana na  Daina. Nikusaidie tafadhali!

“Naitwa Babuu! Ni mwenyeji wa Arusha na nipo hapa kibiashara.

“Ndiyo!”

“Nafanya biashara ndani na  nje ya nchi!” Babuu alijieleza kama mfanyabiashara wa vitu mbalimbali. Alichukua bidhaa nje ya nchi  na kuziingiza nchini. Alihitaji urafiki na Diana katika biashara.

Edward alikuwa ofisini kwake pamoja na wenzake. Aliwasimulia  kila kilichotokea ofisini  kwa Diana. Diana alikubali kushirikiana naye katika biashara. Alitaka kuzoeana naye sana ili arahisishe kazi yake.

Edward aliamini kila kitu kingekwenda sawa. Hakuwa na wasiwasi hata kidogo katika kukamilisha jukumu lake la kumtia hatiani yeyote aliyekuwa na shutuma. Alikuwa ni mzoefu katika kazi yake ya upelelezi.

Kazi ya kumzoea Diana ikaanza mara moja. Diana alimkaribisha hadi nyumbani  kwake na kumtambulisha kwa mshirika wake. Akamfanya kuwa mtu wake wa karibu  sana. Kila jioni walikuwa katika kumbi za starehe na kushauriana naye katika masuala ya kibiashara.

Taratibu Edward akaanza kupata mambo muhimu ya upelelezi wake. Aliwafahamu watu muhimu katika biashara ya dawa  za kulevya. Akaamini haukuwa mbali sana katika kukamilisha upelelezi. Diana alikuwa  ndani ya ofisi yake pamoja na mshirika wake katika biashara. Aliitwa Omary. Alikuwa amempelekea taarifa mbaya mno.  Kwa upande wake ilikuwa ni taarifa mbaya lakini muhimu sana kwa biashara na maisha yao pia. ”Huyu siyo Babuu! Anaitwa  Edward na ni mpelelezi wa FBI. Omary alimwambia Diana ambaye hakuwa ameamini kile alichoambiwa.

“Hapana”! Diana alikataa.

“Diana! Diana! Diana! Huyu kijana ni hatari mno! Ngoja akikuumiza  ndio uthibitishe maneno yangu. Omary akamwambia Diana wakati akiinuka tayari kuondoka. Hakutaka kuendelea kumuelimisha Daina aliyeonekana  kutotaka kuelewa.

Mara baada ya Omary kuondoka  Daina akaacha kufanya kazi nyingine na kutulia. Akaanza kufikiri  namna Babuu anavyoonekana. Hakutaka kuamini kwamba Babuu alikuwa ni mpelelezi. Akaanza kuamini  maneno ya Omary baada ya kupigiwa simu na Godson mshirika wake mkubwa katika biashara. Alimpa taarifa kama ile aliyopewa na Omary.

Ghafla  kichwa kikaanza kuwanga mno. Hasira ikampanda na kuichafua akili yake. Akachoka na kulegea.

Akainua simu ya mezani na kubonyeza namba fulani. Haukupita muda mrefu  sauti ya kike ikasikika kutoka  upande wa pili wa simu.

“Sihitaji kuonana na mtu yeyote yule iwe ni ofisini au binafsi. Usimruhusu mtu.” Aliwambia katibu muhtasi wake. Hakutaka kuonana na mtu yeyote yule. Alihitaji muda wa kupumzisha ubongo wake.

“Huyu atajuta! Kama kweli ni mpelelezi  afadhali angekwenda pengine ila sio kwangu. Atajuta maisha yake yote.” Diana alijiapiza wakati akiwa amejiegemeza  kwenye kiti. Hakutaka tena  kumwona Babuu.

Edward alikuwa ofisini kwake. Kichwani kwake alikuwa na mawazo mengi. Alifikiria namna ya kukamilisha upelelezi wake. Hakupenda kuchelewa kumaliza kesi kwa kipindi kirefu kama hicho.

 Alisikia simu ikiita. Alipoangalia kwenye kioo alikuwa ni Bernard akipiga. Akabonyeza kitufe cha kijani na kuiweka sikioni.

“Hallow Edward!”

“Ndiyo Bernard.” Nimepata taarifa za kusikitisha

kidogo.”

“Taarifa gani?” Edward alihoji.

“Omary amekutwa ndani ya gari lake akiwa amekufa.”

“Eeh”! Edward alishtuka. Akatulia ili apewe maelezo mazuri. Bernard alimwambia Edward kuwa Omary alikutwa amekufa akiwa ndani ya gari lake nje ya ofisi yake. Haikuonyesha kama alipigwa na kujeruhiwa kabla ya kifo chake.

Mwili wake haukuwa na alama yoyote ya kuonyesha kama alipigwa na kujeruhiwa kabla ya kifo chake.

Edward alitoka na kuelekea  katika hospitali ambapo mwili wa Omary ulikuwa umehifadhiwa.

Ilikuwa ni mwendo wa kama saa thelathini  hivi kabla ya kufika mahali mwili wa Omary ulipokuwa umehifadhiwa.    Akamkuta Edward na Imelda wakiwa wakimsubiri.

“Inaonekana hakupigwa wala kujeruhiwa”. Bernard alimwambia Edward.

“Post mortem?” Edward alimaanisha uchunguzi  wa kidaktari kwa mwili wa marehemu.

“Bado haujafanyika”.

“Tusubiri ili tujue ni nini kimetokea”. Edward alitoa agizo. Ilikuwa ni muhimu kufanya uchunguzi wa kitabibu  kufanyika ili kuthibitisha kilichotokea kabla na baada ya maiti ya Omary. Hawakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kusubiri uchunguzi wa madaktari  bingwa.

Mwisho.