Na XINHUA ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Friday, February 17 2012 at 19:51Kwa Mukhtasari
Christian Wulff alijiuzulu baada ya viongozi wa mashtaka kuliomba bunge la Ujerumani limwondolee kinga dhidi ya mashtaka, jambo ambalo lingepelekea yeye kuchunguzwa rasmi kuhusiana na madai ya ufisadi. Anadaiwa kuchukua mkopo kutoka mke wa rafiki yake kwa riba ya chini 2008.
BERLIN, Ujerumani
CHANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel, Ijumaa alieleza masikitiko makubwa kufuatia kujiuzulu kwa Rais Christian Wulff.
Kiongozi huyo alijiuzulu kufuatia mzozo ulitokana na mkopo wa kibinafsi ambao alikuwa ameuchukua.
Nusu saa tu, baada ya Wulff kutangaza kujiuzulu kwake, Merkel, kwenye taarifa alimshukuru rais huyo kutokana na mchango wake na kusema anaheshimu uamuzi wake.
Alisema atashauriana na Serikali, vyama vya kisiasa kutafuta atayechukua wadhifa wa Wulff.
Mashtaka
Wulff, 52, alitangaza kujiuzulu kwake kwenye kwenye televisheni, baada ya viongozi wa mashtaka kuliomba bunge la Ujerumani limwondolee kinga dhidi ya mashtaka, jambo ambalo lingepelekea yeye kuchunguzwa rasmi kuhusiana na madai ya ufisadi.
Wulff, alikuwa mshirika wa karibu wa Merkel, lakini alikabiliwa na shinikizo ilipobainika kuwa alijaribu kuzima ufichuzi wa gazeti la Bild, kuhusu mkopo aliouchukua 2008 kutoka kwa mke wa rafiki yake kwa riba ya chini mno.
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel