Na VICTOR SIELE ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Saturday, February 18 2012 at 19:26Kwa Mukhtasari
BINGWA wa KPL, Tusker FC, italazimika kupigana vita vya kufa kupona ili kupiga hatua katika dimba la Klabu Bingwa Afrika baada ya kukabwa koo na kutoka sare ya 0-0 dhidi ya APR ya Rwanda kwenye mechi kali iliyochezwa uwanjani Nyayo, Nairobi.
BINGWA wa KPL, Tusker FC, italazimika kupigana vita vya kufa kupona ili kupiga hatua katika dimba la Klabu Bingwa Afrika. Hii ni baada ya kukabwa koo na kutoka sare ya 0-0 dhidi ya APR ya Rwanda kwenye mechi kali iliyochezwa uwanjani Nyayo, Nairobi, Jumamosi. Timu hizi zitakutana tena nchini Kigali katika muda wa majuma mawili yajayo.
Katika kipindi cha kwanza Paul Were alitikisa wavu dakika ya 14 lakini refa akaamua alikuwa ameotea. Dakika nne baadaye straika hatari Dennis Mukaisi alionekana kuwashinda nguvu madifenda kwa mbio kabla ya kupokonywa mpira alipokaribia eneo hatari.
Wageni walifanya mavamizi yalimwagika katika dakika za kwanza za kipindi cha pili bila mafanikio kufuatia kazi ya ziada ya madifenda wa Tusker wakiongozwa na Brian Mandela. Ingawa walikuwa na kazi ngumu kuzuia chenga za mastraika wa APR, Iranzi Jean Claude na Olivier Karekezi, Noah Abitch, Isaac Otieno, Joackins Atudo na Mandela walijumuika kuhakikisha ngome na kiungo hakupitiki.
Dakika zilikuwa zikiyoyoma huku matumaini ya kupata bao yakiisha katika kila upande.
APR ilionekana kufunga bao kupitia kona iliyochajwa na John Baptiste katika dakika ya 88 lakini kipa wa Tusker, Boniface Oluoch alikuwa macho kuunyaka.
APR imeshiriki kombe hili kwa miaka minane lakini haijawahi kupita hatua ya kwanza ingawa inajivunia mataji 12 ya Ligi Kuu ya Rwanda, huku Tusker ikiwa imeshinda KPL mara tisa. Wanamvyo wanashiriki dimba hili kwa mara ya saba ambapo wamefika hatua ya raundi ya pili, waliposhiriki miaka kumi iliyopita. Wamebanduliwa katika raundi ya kwanza katika makala sita.
Mechi kati ya mabingwa wa FKL, Gor Mahia na Ferroviaro ya Msumbiji ilitarajiwa kuchezwa baadaye.
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel