Serikali yaondoa hofu kuhusu ardhi Lamu

Katibu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Cyrus Njiru

Picha/PHOEBE OKALL Katibu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Cyrus Njiru akihutubia wanahabari afisini mwake jijini Nairobi, Februari 8, 2010. 

Na GALGALO BOCHA  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Friday, February 10  2012  at 16:22

Kwa Mukhtasari

Katibu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Cyrus Njiru, ameyalaumu mashirika ya kijamii na wanasiasa kwa kuwapotosha wakazi hao kwamba maelfu ya watu wataondolewa kwenye ardhi yao ya jadi itakayotumiwa kwa ujenzi wa bandari hiyo.

 

SERIKALI imewahakikishia wakazi wa Lamu kuwa hakutakuwa na utwaaji wa lazima wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Lamu.

Katibu wa wizara ya Uchukuzi, Dkt Cyrus Njiru, ameyalaumu mashirika ya kijamii na wanasiasa kwa kuwapotosha wakazi hao kwamba maelfu ya watu wataondolewa kwenye ardhi yao ya jadi itakayotumiwa kwa ujenzi wa bandari hiyo.

“Watu wa Lamu wamepotoshwa ndiposa wameshindwa kuelewa msimamo wa serikali. Lakini baada ya mkutano na wawakilishi na viongozi wao, tumeweka wazi kwamba serikali haitachukua ardhi ya mtu kwa lazima ili kujenga bandari,” Dkt Njiru akaambia Taifa Leo kwa simu baada ya kikao hicho katika ukumbi wa Lamu.

Dkt Njiru alisema bandari hiyo itajengwa ndani ya maji kupunguza gharama ya kujenga sehemu za kuegesha meli ambapo kutakuwa na uchimbaji mdogo wa kupanua kina cha maji kwa ajili ya kuegesha meli kubwa kubwa.

“Sehemu ya bara itatumiwa kwa ujenzi wa barabara na mijengo mingine ya bandari na watakaoathiriwa watalipwa ridhaa kuambatana na sheria. Ninafuraha kila mkazi aliondoka mkutanoni akiwa ameelewa na tayari wamekubali kuunga mkono ujenzi wa bandari,” akaeleza.

Ajira na uchumi

Mkurugenzi mkuu wa bandari ya Mombasa (KPA), Bw Gichiri Ndua na Mkurugenzi Mkuu, Bi Nancy Karigithu walikuwa miongoni mwa wakuu wa serikali walioandamana na Dkt Njiru.

Dkt Njiru aliwaeleza wakazi wa Lamu kuwa bandari hiyo itazalisha maelfu ya nafasi za ajira na kuimarisha uchumi wa nchi ikiwa mbali na kutimiza malengo ya ruwaza ya mwaka wa 2030. 

Mwenyekiti wa baraza la wilaya ya Lamu, Bw Abdul Kassim Ahmed alionya serikali kuwa wakazi wataendelea kupinga mradi huo endapo haitatimiza ahadi zake kuhusu utoaji hati miliki za ardhi kwa wakazi wa jadi wa Lamu.

“Sote tunaunga mkono bandari. Lakini wakazi wapewa hati miliki ya ardhi zao kabla ya kuanzisha ujenzi wa bandari ili waweze kuzungumza na waekezaji wanaotafuta ardhi za kuanzisha viwanda miongoni mwa biashara zingine,” akaeleza.

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel