Apigwa na kuumizwa na mke wa kakake

Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka.

Picha/MAKTABA Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka ambaye amekuwa akitetea wanaume akihutubia wanahabari Desemba 17, 2009. 

Na JAMES KARIUKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Friday, February 17  2012  at 18:19

Kwa Mukhtasari

Bw Stephen Macharia aliyelazwa hospitalini alisema alikuwa akizozana na kakake kuhusu watakavyolima shamba la wazazi wao.

 

MWANAUME amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nyandarua akiwa na majeraha kichwani na mkononi, akidai aliyapata baada ya kupigwa na mke wa kakake.

Bw Stephen Macharia akizungumza kwa maumivu kutoka kitanda cha hospitali, aliambia Taifa Leo kuwa alikuwa akizozana na kakake kuhusu watakavyolima shamba la wazazi wao.

“Nikiwa sina habari, mke wa kakangu aliingilia kati na kuanza kunishambulia kwa chuma kichwani, mikononi na miguuni. Kakangu naye alienda kwake nyumbani akarudi akiwa na panga na kumsaidia mkewe kunikata,” akasema.

Alisema kwamba aliwachwa akiwa ameanguka chini na kakake akaamuru tingatinga alilokuwa ameenda nalo hapo shambani kulima liondoke.

“Nimepiga ripoti katika kituo cha polisi cha Huho-ini hapa wilayani Nyandarua Magharibi, lakini kakangu na mkewe wangali huru,” akalalama.

Kisa hicho kilitokea katika eneo la Silibwet.

Mzozo kuhusu shamba

Bw Macharia alisema kwamba mzozo huo kuhusu shamba uliwalazimisha nduguze wengine kuondoka, wakihofia kuwa kaka yao na mkewe wangelitekeleza vitisho vyao kuwa 'watatumaliza’.

“Alitimiza vitisho vyake kwa kunishambulia. Kama hakutachukuliwa hatua, nahofia kuwa huenda akarudia jambo hilo, na safari hii anaweza kuua mtu,” akasema.

Mwanaume huyo mwenye watoto watatu, alisema pia alipata majeraha ya ndani ya mwili, hasa kifuani na mgongoni, kutokana na kichapo cha 'nguvu’ alichopokea kutoka kwa kakake na mumewe.

Tukio hilo la Nyandarua linafuatia msururu wa visa vya wanaume kushambuliwa na wanawake katika maeneo ya Nyeri, Ruiru, Kiambi, Bungoma na Kisii.

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel