HABARI ZA SIASA

Uhuru na Ruto wasema hawajamtenga Kalonzo

Bw Ruto na Bw Musyoka

Picha/JENNIFER MUIRURI Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka (kulia) ajumuika na Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto baada ya mkutano katika hoteli ya Norfolk, Nairobi Februari 17, 2012. 

Na JAMES KARIUKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Saturday, February 18  2012  at 17:46

Kwa Mukhtasari

Wakihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo mbali mbali ya Nyandarua, wawili hao na wafuasi wao walisema lengo lao ni kudumisha umoja na kuhakikisha Wakenya wanapata viongozi bora.

NAIBU Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na Mbunge wa Eldoret Kaskazini Bw William Ruto, Jumamosi walisema hawana nia ya kumtenga Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka.

Wakihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo mbali mbali ya Nyandarua, wawili hao na wafuasi wao walisema lengo lao ni kuhakikisha Wakenya wanapata viongozi bora.

Walisema wataungana kuhakikisha Wakenya hawapigani tena kama ilivyokuwa mwaka 2008, ambapo watu wengi waliuawa kutokana na ukabila.

“Kama ni Uhuru, Kalonzo, Murungi, Wamalwa, Ruto au yeyote mwengine, kuweni tayari kuungana nasi ili tumpe nafasi ya kuwapa Wakenya huduma zinazoambatana na sera nzuri,” alisema Bw Ruto.

Aliambia wananchi waliojitokeza katika maeneo ya Ndaragwa, kwa Kung’u, Mairo Inya, Nyahururu, Ol Jororok na Ol Kalou mjini kuwa uongozi wao utashughulikia uhaba wa ajira miongoni mwa vijana na kuwapa wakulima pembejeo za kilimo, miongoni mwa huduma nyingine muhimu kwa wananchi.

Wawili hao waliandamana na wabunge 20 kusema kuwa G7 ni mtandao mmoja usioweza kuvurugwa na yeyote.

Madai ya kutengwa

Mbunge wa Horr Kaskazini Bw Chachu Ganya, aliongoza wabunge wengine kusema kuwa makamu wa Rais atakuwa sehemu ya kundi hilo.

“Madai kuwa tumemtenga Kalonzo ni ya vyombo vya habari. Kundi letu la G7 linahitaji kura kutoka kwa kila mtu na hatuwezi kumtenga Kalonzo,” akasema.

Mwenzake wa Dujis Bw Aden Duale, alisema kwamba ni viongozi chini ya G7 pekee watakaotambuliwa na viongozi hao.

Chini ya mwito wa “Tuko Pamoja” Waziri Msaidizi Mwangi Kiunjuri aliwaomba vijana wachukue vitambulisho na kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura.

Alisema si sawa kwa vijana ambao ndio wenye kauli katika uchaguzi, kuwaachia watu wengine kuwachagulia viongozi.

Lakini Bw Kenyatta aliamua kuwalaumu viongozi fulani aliodai wanatumiwa na Wazungu kushinikiza kesi iendelee katika mahakama ya ICC.

“Kuna Wazungu wanaotumiwa na wanasiasa fulani ili watuzuie kuwania urais.

Nataka watambue kuwa ni Wakenya walio na kura na wala si wazungu ambao tuliwafukuza nchini wakati wa kupata uhuru wetu,” akasema.

Kesi za ICC
Bw Kenyatta alisema kuwa viongozi hao wanaotumia ICC kuwazuia kushiriki kwenye uchaguzi wa urais ni waoga wa kushindwa.

“Tuliwafukuza wakoloni kutoka nchi yetu na sasa sisi ni taifa huru linalojisimamia.

Hoja kwamba tunaogopa Kenya kutotambuliwa na jamii ya kimataifa iwapo mimi na Ruto tutawania urais ni za kikoloni,” akasema.

Aliwahimiza Wakenya wasikubali njama za kuwazuia kuwania urais, huku akisema kuwa ni viongozi walafi pekee wasiokubali kushindwa.

Baadhi ya wanasiasa walioandamana nao ni wabunge Kazungu Kambi (Kaloleni), Jeremiah Kioni (Ndaragwa), William Kabogo (Juja ), Abdul Bahari (Isiolo) na Mike Mbuvi 'Sonko’ wa

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel