HABARI ZA SIASA
Picha/MAKTABA Mwenyekiti wa Chama cha Shule za Kibinafsi, Bw John Mwai (kushoto) akiwa na Mwekahazina wa chama hicho, Bw Kabiru Ndiritu, kwenye kikao na wanahabari Januari 18, 2012.
Na WAANDISHI WETU ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Saturday, February 18 2012 at 18:7Kwa Mukhtasari
Wazazi wanahamisha wanafunzi kutokana na mfumo wa uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, ambao kwa miaka mitatu sasa umeonekana kuwapendelea wanafunzi wa shule za umma.
WAZAZI wengi wameanza kuwaondoa watoto wao kutoka shule za msingi za kibinafsi na kuwapeleka kwa zile za umma.
Chama cha shule za kibinafsi na kile cha wazazi, vimekiri kuwa kuna uhamishaji wa kiwango cha juu wa wanafunzi, hasa wa madarasa ya saba na nane.
Shule nyingi za msingi za umma sasa zina msongamano mkubwa wa wanafunzi.
Hali hii inatokana na mfumo wa uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, ambao kwa miaka mitatu sasa umeonekana kuwapendelea wanafunzi wa shule za umma.
Baadhi ya wazazi wameshutumiwa kwa kuungana na walimu wakuu wa shule za msingi za umma, ili watoto wao wasajiliwe kufanya mitihani yao ya KCPE huko, licha ya kuendelea kusoma katika shule za msingi za kibinafsi hadi mtihani wa KCPE uanze.
Usajili wa wanafunzi si siri
Katibu Mkuu wa Chama cha Wazazi (KNAP), Bw Musau Ndunda, alisema usajili wa wanafunzi kutoka shule za kibinafsi katika shule za umma sio siri.
“Sera ya serikali kuwapa wanafunzi wa shule za umma kipaumbele wakati wa kujiunga na kidato cha kwanza imewasababisha wazazi wengi kuungana na walimu wakuu ili watoto wao wasajiliwe kufanya mitihani yao, huku wakiendelea kusoma katika shule za kibinafsi,” alisema.
Bw Ndunda aliambia Taifa Jumapili kuwa, licha ya hatua hii kukiuka sheria, wazazi hawapaswi kulaumiwa kwani kila mmoja ana haki ya kumtafutia mwanawe masomo mema.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule za kibinafsi KEPSA, Bw John Mwai, alisema mfumo huu mpya pia umesababisha wazazi wengi kuwahamisha watoto wao katika shule za umma za malazi.
Karo imezidi
“Nyingi ya shule hizi ni za hali ya juu na hata karo imezidi inayolipwa katika shule nyingi za kibinafsi. Tofauti na shule nyingi za kibinafsi, shule hizi kama Nairobi Primary, Muthaiga Primary na Nyeri Complex zina vifaa bora na hivyo zinatoa fursa kwa wanafunzi kukubaliwa katika shule za kitaifa,” asema.
Kulingana na Bw Mwai, huenda hatua hii ikaleta misongamano katika shule hizi na hata kuathiri kiwango cha masomo.
Alhamisi iliyopita, katibu katika Wizara ya Elimu Prof James Ole Kiyiapi aliunda jopo kazi litakaloangalia upya mfumo huo wa uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Ripoti za Timothy Kimei, Pauline Ongaji na Simon Siele
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel