Na LUCY KILALO ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Monday, February 20 2012 at 20:21Kwa Mukhtasari
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Ipsos Synovate, asilimia 32 iliidhinisha ugombeaji wa Bw Kenyatta akiwa na Bw Ruto ikilinganishwa na asilimia 14 iwapo Bw Kenyatta atamchagua Bw Musyoka kama mgombeaji mwenza.
WAKENYA wengi wangependa Naibu Waziri Mkuu, Bw Uhuru Kenyatta awanie urais akiwa na Mbunge wa Eldoret Kaskazini, Bw William Ruto kama mgombeaji mwenza chini ya muungano wa G7, kura ya maoni imeonyesha.
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la utafiti la Ipsos Synovate, asilimia 32 iliidhinisha ugombeaji wa Bw Kenyatta akiwa na Bw Ruto ikilinganishwa na asilimia 14 iwapo Bw Kenyatta atamchagua Bw Musyoka kama mgombeaji mwenza.
Wagombeaji wengine wanaopendelewa katika kura hiyo ni Bw Musyoka na Bw Eugene Wamalwa pamoja na wagombeaji wengine wakichukua asilimia nane.
Utafiti ulifanywa kati ya Januari 21 na Februari 2 mwaka huu, lakini haukutolewa mapema kwa sababu uligusia masuala yaliyohusiana na Bw Kenyatta na Bw Ruto.
Raila bado aongoza
Hata hivyo, Waziri Mkuu Raila Odinga bado anaendelea kuwa mgombeaji urais maarufu zaidi akiwa na asilimia 31 na kufuatwa na Bw Kenyatta akiwa na asilimia 24 naye Bw Musyoka na 10. Matokeo hayo yalionekana kuwa sawa na utafiti uliokuwa umefanywa awali.
Wengi wa watu zaidi ya 1,500 waliohojiwa watampigia kura Bw Odinga iwapo kutakuwa na marudio ya uchaguzi kati yake na mmoja wa wagombezi wa urais.
“Bw Odinga atapata asilimia 44 ilhali Bw Kenyatta atapata 42 katika marudio ya uchaguzi. Na ikiwa ni baina ya Bw Odinga na Bw Kalonzo, watakuwa na asilimia 44 na 41. Uchaguzi ukiwa kati ya Raila na Martha Karua, watakuwa na asilimia 43 na 33 na ikiwa ni kati yake na Bw Ruto, atapata asilimia 50 dhidi ya 33,” kura hiyo ya maoni ilionyesha.
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel