Nukuu muhimu alizotoa marehemu Michuki

John Michuki akiwa kijana.

John Michuki akiwa kijana. 

Na ANTHONY NYONGESA  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 14:41

Kwa Mukhtasari

Marehemu Michuki alijulikana kwa hotuba na taarifa zake zilizojaa uzito wa maneno na maana.

 

“Tukijua wewe unataka kuingia kwa Wakikuyu bila ya kupitia kwa Uhuru wa Kenyatta, sisi tutatwanga wewe kisiasa. Uhuru wa Kenyatta ndio kiongozi wa Wakikuyu. Mtu yeyote anayetaka kuzungumza na Wakikuyu, azungumze na Uhuru na Uhuru atatuambia ,” ndio matamshi ya mwisho ya kisiasa ya aliyekuwa waziri wa mazingira John Michuki akiwa Murang’a Oktoba 2011

Aliwapuuza viongozi wengine wa eneo hilo wanaompinga Uhuru huku akisisitiza kwamba katika uchaguzi mkuu ujao, Uhuru ndiye anayepasa kuungwa mkono.

“Ukimchokora nyoka, kuwa tayari kuumwa na nyoka huyo,” ni msemo ambao kamwe hautasahaulika kwa urahisi ambapo Michuki alikuwa akiwajibu wanahabari baada ya afisi za Standard Group kuvamiwa na magaidi wa kukodishwa.  Ilikuwa Machi 2006. Matamshi haya yaliwakera mno wanaharakati na mabalozi waliomtaja Michuki kiongozi kiimla.

“Wacha niseme hapa wazi wazi kwamba aliyekuwa mbunge wa Kabete Paul Muite anayo matatizo chungu nzima yaliyompelekea kupoteza kiti chake cha ubunge. Asijaribu kutafuta nafasi kwa magazeti kwa kujihusisha nami,” waziri Michuki akimwonya Muite mnamo Aprili 2009 aliyedai kwamba maisha yake yalikuwa hatarini

 

“Ati kwa maana unamilki matatu chache sasa unataka kujionea mtu 'special’? Haiwezekani kabisa,” Michuki akiwaonya wanaoendesha biashara ya matatu nchini mnamo Agosti 2008

 

“Hatuna starehe na muda wa kupoteza kwa kuendelea kuhairisha mipango ya kuboresha mazingira. Mataifa yanayostawi yanapasa kuweka makubaliano mengine sawa na yale ya Kiyoko ili kutulinda kimazingira kati ya 2013 na 2017,” alisema Michuki Desemba 2011 alipokuwa jijini Durban, Afrika Kusini kwenye kongamano la mabadiliko katika hali ya anga. Hii ni moja wapo ya kazi ya mwisho ambayo aliitekeleza waziri Michuki kabla ya kuelekea Uingereza kwa matibabu.

 

“Nilipokuwa kwenye wizara ya uchukuzi, niliwatafuta maafisa wa trafiki mimi mwenyewe. Haijalishi ilikuwa saa ngapi au siku gani. Wakati mwingine nilichukuliwa adui na maafisa wa na wenye matatu,” alieleza waziri waziri Michuki mwishoni mwa 2009 alipoingia katika wizara ya mazingira.

 

“Watu wa kuomba omba hawana namna. Kwa kweli sisi tumefanywa watu wa kuomba. Tumefanywa watu wa kuomba omba katika hali ambayo inastahili kuwa haki yetu,” alieleza akilalamikia mataifa yaliyostawi kuyanyanyaza yale yanayokuwa kwenye kongamano OneClimate at COP15 jijini Copenhagen mnamo Desemba, 2009.

 

“Nimezungumza kwenye jukwaa. Nimezungumza vya kutosha, wewe ulikuwa? Nyinyi wanahabari mnashangaza sana,”- akimtania mwanahabari wa CNN aliyetaka kuzungumza naye baada ya kongamano OneClimate at COP15 jijini Copenhagen mnamo Desemba, 2009.

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel