Na CHARLES MWANIKI ( email Mwandishi)
Imepakiwa - Wednesday, February 22 2012 at 19:24Kwa Mukhtasari
Bw Patrick Kimaru Mwangi, aliambia Hakimu Mkuu Mkazi wa Nyeri, Bi Joan Wambilyanga kwamba alimsamehe mkewe, Bi Eunice Wairema Gaitho, baada ya kuombwa msamaha na kuhakikishiwa kwamba asingechapwa tena.
MWANAUME ambaye alikuwa wa kwanza kujitokeza hadharani kwa kudai kuchapwa na mke wake sasa ametupilia mbali kesi dhidi ya mwanamke huyo mahakamani.
Bw Patrick Kimaru Mwangi, aliambia Hakimu Mkuu Mkazi wa Nyeri, Bi Joan Wambilyanga kwamba alimsamehe mkewe, Bi Eunice Wairema Gaitho, baada ya kuombwa msamaha na kuhakikishiwa kwamba asingechapwa tena.
Bi Wairema alishtakiwa Januari 23 kwa madai ya kupiga na kumuumiza Bw Kimaru mnamo Januari 1, katika kijiji cha Ngangarithi, Nyeri.
Wakati Kiongozi wa Mashtaka, Inspekta Bernard Wamalwa alisema kwamba alikwa tayari kuendeleza kesi, Bi Wairema aliomba kuzungumza, na kueleza kwamba mumewe, ambaye ni msanii mjini Nyeri, alikuwa tayari kuondoa mashtaka hayo dhidi yake.
Hakushurutishwa
Alipoitwa mbele ya korti kuthibitisha ukweli huo, Bw Kimaru alisema kwamba hakushurutishwa na yeyote kuondoa kesi hiyo, bali alifanya hivyo kwa hiari yake.
“Mke wangu ameniomba msamaha na kuniambia kwamba hatarudia kosa hili. Nimekubali kwani yeye ni mke wangu na sijashurutishwa na yeyote kuondoa mashtaka haya,” akasema Bw Kimaru.
Kwenye kesi nyingine, watu watatu waliioshtakiwa kwa madai ya wizi wa mali kwenye vyumba vya hoteli ya kifahari ya Outspan, wataendelea kuzuiliwa kwenye Kituo cha polisi cha Nyeri hadi Ijumaa kufuatia ombi kutoka kwa upande wa mashtaka.
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel