#MchujoJubilee: Matukio yote kadri yalivyojiri

Raphael Tuju

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju akihutubia wanahabari. PICHA/ LEONARD ONYANGO 

Na FAUSTINE NGILA

Imepakiwa - Thursday, April 20  2017 at  20:34

Kwa Mukhtasari

KIVUMBI kikubwa kinatarajiwa wakati wa shughuli ya mchujo ya Chama cha Jubilee Ijumaa Aprili 21.

Hapo Jumatano EACC iliwaonya wanasiasa na wapiga kura dhidi ya kujihusisha katika visa vya hongo, watakaonaswa watakumbana na makali ya sheria.

Kufuatia uamuzi wa chama cha Jubilee kutimua maafisa 73 waliokuwa wameteuliwa kusimamia zoezi la mchujo, chama hicho kilijisifu kwamba ndicho chama kinachofanya mambo kwa usawa na haki na kuwa ni mkakati wa kuzima wizi mchujoni.

Rais hapo Alhamisi aliwaonya vikali watakaojaribu kuzua ghasia kwenye mchujo huo kwamba hatachelewa kuwaadhibu ipasavyo.

SWAHILIHUB inakuletea matukio yote kadri yanapochipuka katika vituo mbalimbali vya kupiga kura.

 

20/4/2017:

6.00 PM Mwaniaji tiketi ya JP ya ugavana wa Tharaka Nithi Bw Petkay Miriti asema hatakubali matokeo akishindwa kesho na Muthomi Njuki. Anasema mbunge huyo alifumaniwa nyumbani kwake usiku wa Jumatano akitia alama karatasi za kura, madai ambayo Njuki ameyakanusha

6.17 PM Kamanda wa Polisi eneo la Meru Nelson Taliti apokea masanduku ya kura za mchujo katika ofisi yake.

21/4/2017

6.39 AM Wapiga kura wafika kwenye lango katika kituo cha kura cha Shule ya Upili ya Nakuru. Kituo bado hakijafunguliwa.

6.42 AM: Mvua kubwa iliyonyesha katika kaunti ya Kirinyanga yachelewesha vifaa vya kupiga kura. Aidha, Mratibu wa eneo hili Hudson Aluvansa asema mchakato unaendelea vyema.

6.44 AM: Wapiga kura wazidi kusubiri kufunguliwa kwa kituo cha Shule ya Msingi ya Mbiiti, kaunti ya Murang'a.

6.46 AM: Wapiga kura warudi nyumbani baada ya kusubiri kufunguliwa kwa kituo cha Shule ya Msingi ya Meru bila mafanikio. Lango la shule bado limefungwa.

6.59 AM: Taharuki yatanda katika kituo cha ukumbi wa Eldama Ravine mjini baada ya baadhi ya karatasi za kura za ugavana kukosekana. Eneo hili ni ngome ya Stanley Kiptis anayemenyana na gavana Cheboi. Wapiga kura wameapa kutoshiriki mchujo iwapo karatasi hizo hazitatolewa, wanamshuku gavana Cheboi

7.10 AM: Mchujo wa Bomet waahirishwa hadi Jumanne Aprili 25, 2017

7.16 AM: Sintofahamu katika kituo cha Ukumbi wa MV Patel mjini Eldoret baada ya ukosefu wa vifaa vya kura vya kutosha. Wapiga kura walia hoi kuwa ni njama ya mapema ya kuiba kura. Wakataa kupiga kura hadi pale vifaa vyote vitawasilishwa. Kituo hiki kina wapiga kura 20,000 lakini karatasi za kura zilizofika ni 3,000

7.26 AM: Mchakato wa kupiga kura bado haujaanza katika vituo vingi kaunti ya Kiambu. Kisa na maana, maafisa bado hawajafika vituoni

7.38 AM: Polisi wabishana na wapiga kura walioghadhabishwa na kucheleweshwa kwa mchakato katika kituo cha MV Patel, wadi ya Huruma, eneobunge la Turbo, kaunti ya Uasin Gishu

7.40 AM: Mwaniaji udiwani wadi wa Turi, eneobunge la Molo Bw Vincent Kilonzo alalamikia kucheleweshwa kwa upigaji kura. Uchaguzi ulifaa kuanza saa kumi na mbili asubuhi

7.46 AM: Vijikaratasi vyasambazwa katika eneobunge la Tetu vikichochea wapiga kura kutompigia kura wakili Gichuhi Mwangi. Ujumbe kwenye vijikaratasi hivyo wasema wakili huyo ni muuzaji sugu wa vileo hatari. Vyaongeza kuwa Bw Mwangi ni mlaghai, mnyakuzi a ardhi, ni mkazi wa Othaya pamoja na kuwa wakili na mfuasi sugu wa Raila Odinga.

7.50 AM Chama cha Jubilee chatoa taarifa kuwa kimeweza kufikisha vifaa vya kura katika vituo vyote vinavyoshiriki mchujo 

7.52 AM: Masanduku ya kura yafika katika vituo kadha vya kupiga kura katika kaunti ya Kiambu

8.06 AM Vifaa vya kupiga kura bado havijafika katika kituo cha Shule ya Msingi ya Tumutumu, eneobunge la Mathira, Nyeri 

8.14 AM Wapiga kura walalamikia kucheleweshwa wa zoezi hilo katika kituo cha Race Course, Kapseret

8.21 AM Upigaji kura waanza katika kituo cha Shule ya Msingi ya Arap Moi, eneobunge la Ainabkoi

8.24 AM Maafisa wa usalama katika kituo cha Ukumbi wa Thika mjini. Vifaa vya kupiga kura bado havijafika katika vituo vingi katika maeneobunge ya Thika na Ruiru

8.31 AM Wapiga kura mjini Thika wadai hatua ya kuhesabia kura katika Ukumbi wa Thika ni (ofisi ya awali ya gavana) ni njama ya kuiba kura 

8.36 AM Wapiga kura wazidi kuishiwa na subira katika kituo cha GK Prison, wadi ya Oloosirkon Sholinke, Kajiado Mashariki. Wasema wamekerwa na kucheleweshwa kwa vifaa 

8.37 AM Gavana wa Baringo Benjamin Cheboi afukuzwa na wapiga kura wenye hamaki katika kituo cha  Eldama Ravine. Waimba nyimbo za 'Cheboi lazima aende' 

8.42 AM Polisi wadhibiti hali katika eneo la Shule ya Upili ya Oloolaiser, Ngong. Lori lililobeba karatasi za kura lasimamishwa hapa. Wawaniaji wadai kuna njama ya wizi wa kura maanake karatasi hizo zilifaa kupekekwa katika kituo cha kuhesabu kura Kajiado mjini

8.52 AM: Foleni ndefu katika kituo cha Railway mjini Nakuru. Upigaji kura haujaanza

9.00 AM Mwaniaji kiti cha Mwakilishi Mwanamke Gladys Shollei alalamikia matayarisho duni ya chama cha Jubilee kwa mchujo katika kituo cha MV Patel

9.02 AM Maafisa watayarisha masanduku ya kura kusafirishwa hadi vituoni katika Ukumbi wa Molo

9.02 AM Maafisa watayarisha masanduku ya kura kusafirishwa hadi vituoni katika Ukumbi wa Molo

9.03 AM Mwaniaji ubunge Turbo Bw Kevin Okwara ajaribu kuwatuliza wapiga kura waliotamaushwa na matayarisho duni kituoni MV Patel

9.03 AM Masanduku ya kura yafika katika vituo vichache Gatundu Kusini na Kaskazini, na Thika Mjini

9.05 AM Masanduku ya kura yafika katika kituo cha Ukumbi wa Thika Mjini

9.07AM Sajili ya wapiga kura kituo cha Kahuti-ini, Mathira imepotea. Sintofahamu imetanda mjini Karatina

9.10 AM Ofisi ya Jubilee kaunti ya Nandi yabandikwa posti za CCM mchujo ulipositishwa. Wafuasi wataka kuhamia CCM na KANU

9.11 AM Vifaa vya kupiga kura vyaanza kusambazwa hadi vituoni katika Ukumbi wa Menengai mjini Nakuru

9.15 AM Wapiga kura watishia kugomea mchujo katika kituo cha Shule ya Msingi ya Mau, mchakato umechelewa

9.19 AM Vifaa vya kupiga kura vyawasili kituoni Shule ya Msingi ya Uasin Gishu

9.31 AM Mwaniaji Thika Morris Mburu asema kucheleweshwa kwa mchakato wa kura kutalazimisha muda kuongezwa

9.44 AM Mwaniaji ugavana Kiprop Buzeki adinda kupiga kura akilalamikia ukosefu wa karatasi za kutosha

9.45 AM Mpiga kura achoshwa na kusubiri vifaa vya kura, alala kituoni Shule ya Msingi ya Wangige, Kiambu

9.47AM Kina mama wasubiri upigaji kura kuanza katika kituo cha Shule ya Msingi ya Tayari, Molo

9.47AM Kina mama wasubiri upigaji kura kuanza katika kituo cha Shule ya Msingi ya Tayari, Molo

9.49 AM Hali ilivyo katika kituo cha Mafunzo ya Wakulima Kaguru, Imenti Kusini

9.52 AM Ghasia zazuka mjini Thika baada ya masanduku ya ziada kuonekana yakiingizwa ofisini Ukumbi wa Thika

9.53 AM Masanduku ya kura yalindwa na polisi nje ya Ukumbi wa Thika Mjini

10.00 AM Upigaji kura bado haujaanza katika kituo cha Oloolaiser, Kajiado Kaskazini

10.14 AM Polisi wanasa gari ndogo lililojaa mapanga na marungu katika kituo cha Shule ya Msingi ya Ihururu,Tetu, Nyeri. Washukiwa wawili wamekamatwa, asema Naibu Kamishna Herman Shambi

10.22AM Mwaniaji kiti cha Mwakilishi Mwanamke Nyandarua alalamika jina lake limetiwa alama kwa karatasi za kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Huruma, Ol-Kalou

10.33AM Wapiga kura katika kituo cha Kandenye, Kuresoi Kaskazini bado wanasubiri vifaa vya kupiga kura