Nitampigia debe Uhuru mpende msipende - Waziri Sicily Kariuki

Bi Cecily Kariuki

Waziri wa Utumishi wa Umma, Vijana na Masuala ya Jinsia Bi Sicily Kariuki akihutubu awali. Picha/ HISANI 

Na CHARLES WANYORO

Imepakiwa - Monday, June 19   2017 at  07:35

Kwa Mukhtasari

WAZIRI wa Huduma za Umma na Jinsia Sicily Kariuki ameapa kuendelea kumpigia debe Rais Uhuru Kenyatta huku akisema kuwa ana haki ya kuwafahamisha wapigakura kuhusu mafanikio na miradi ambayo imetekelezwa na serikali.

 

Bi Kariuki jana alisema kuwa hajavunja sheria kwa kutumia mikutano ya kisiasa kuwaelezea Wakenya maendeleo yaliyotekelezwa na serikali.

Akizungumza katika soko la New Site wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusambaza chakula cha msaada inayofahamika kama 'Huduma Mashinani’, Bi Kariuki alisema haendeshi kampeni zake mwenyewe.

“Sitanyamaza kwa sababu mimi siwanii kiti chochote. Katiba inapiga marufuku mawaziri kujipigia debe wao wenyewe. Mimi siwanii kiti chochote na ninampigia debe Rais kenyatta. Nafahamu kilicho chema kwa ajili ya nchi,” akasema.

Bi Kariuki aliyekuwa ameandamana na Mwakilishi wa wanawake wa kaunti, Bi Rose Mitaru, alisema alikuwa ameenda kukutana na wakazi kabla ya ziara ya rais wiki ijayo.