http://www.swahilihub.com/image/view/-/3939910/medRes/1649561/-/lcc94q/-/TWI.jpg

 

#TZvsKE: Wakenya waibuka washindi wa mkaangano dhidi ya Watanzania mtandaoni

Mojawapo ya picha mnaso zilitumwa katika mtandao wa Twitter Mei 24, 2017 kwenye mkaangano baina ya Wakenya na Watanzania. Picha/ HISANI  

Na WANDERI KAMAU

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  12:45

Kwa Muhtasari

WAKENYA Jumatano waliwachachura vikali Watanzania katika mtandao wa Twitter kwa kuwataja kama “duni” kwenye vita vya mtandaoni vyenye anwani #TZvsKE.

 

Aidha, Wakenya waliwakejeli wenzao kwa “kutoufahamu usasa”, kwa mfano ujuzi wa lugha ya Kiingereza.

Kwa mfano, Mkenya Kelvin Otiende alisema: Mtanzania atakwambia “Nipe kofia mbili nyeupe” wakati anaagiza pombe aina ya ‘Whitecap’ kwa Kiingereza.

Picha nyingine ilionyesha Rais Uhuru Kenyatta akisalimia hewa, kumaanisha kwamba hakuna Mtanzania yeyote anayefahamu Kiingereza.

Captain Machuks, aliwasuta Watanzania kwa kuweka video ya mtu akila ‘Pizza’ akiifinya kama ugali, akimtaja kama “Mtanzania wa kwanza kula mlo huo.”

Mose Ax, aliisifu Kenya kwa kutumia Simba kama alama yake ya kitaifa,huku Tanzania ikitumia Twiga. “Hii inamaanisha Wakenya ni shujaa.”

Katika ujumbe mwingine, Solange Mbunde aliwakejeli Watanzania kwa kufanya mambo polepole, akisema kwamba “Huenda mtu akastaafu nchini Tanzania akingoja kuhudumiwa.”

Wakenya pia waliwakabili Watanzania kwa kujisifu kwamba thamani ya pesa za Kenya ni ya juu, ikilinganishwa na ya Tanzania.

Hata hivyo, Watanzania waliwakabili Wakenya kwa kuwaambia wasuluhishe changamoto zinazowakabili kwanza, kama ukosefu wa Unga.

“Wakenya kwanza wajaze matumbo yao,” alisema Idriss Sultan.

Kijumla, Wakenya walionekana kuibuka washindi katika mkaangano huo mkali, kwani ni Sultan pekee aliyewajibu Wakenya.