http://www.swahilihub.com/image/view/-/1498636/medRes/389324/-/tyo3pdz/-/KilelePC.jpg

 

Watu 11 wauawa kwenye shambulio Tana River

Samuel Kilele

Samuel, Kilele, PC, Pwani 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Friday, September 7  2012 at  09:51

Kwa Muhtasari

Watu 11 wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa alfajiri katika shambulio linalodaiwa kuwa la ulipizaji kisasi katika kaunti ya Tana River.

 

WATU 11 wameuawa alfajiri katika shambulio linalodaiwa kuwa la ulipizaji kisasi katika kaunti ya Tana River.

Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, watu 10 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitalini.

Shambulio hilo lililotokea kijiji cha Chamwanamuma, eneo la Tarassa limetekelezwa baada ya wiki kadha za utulivu kufuatia shambulio mbaya katika kijiji cha Riketa lililopelekea kuuawa kwa zaidi ya watu 50.

Katika shambulio la Ijumaa alfajiri, ng’ombe 300 na mbuzi 400 pia waliibwa.

Walioshuhudia walisema milio ya risasi ilitanda hewani huku nyumba zikiteketezwa katika kijiji hicho.

Siku chache zilizopita, utawala wa mkoa ulikuwa umewahakikishia wakazi kwamba usalama umeimarishwa. Rais Kibaki katika hotuba yake wakati wa kufuzu kwa maafisa wa polisi katika chuo cha Kiganjo, Nyeri alionya kuwa wanaochochea jamii watachukuliwa hatua kali.

Maelezo zaidi kufuata.