http://www.swahilihub.com/image/view/-/1864872/medRes/518856/-/1359dj9z/-/Nakuru.jpg

 

Askari ashtakiwa kwa kuharibu kipakatalishi cha mpenziwe

Nakuru

Mji wa Nakuru. Picha/SULEIMAN MBATIAH 

Na JAMES KARIUKI

Imepakiwa - Tuesday, July 16  2013 at  10:16

Kwa Muhtasari

Polisi mmoja wa utawala mjini Nakuru Jumatatu alishtakiwa kwa kosa la kuharibu kipakatalishi akidai mpenziwe anakitumia kupokea jumbe za mapenzi kutoka kwa wanafunzi wa chuo Kikuu cha Egerton. 

 

ASKARI mmoja mjini Nakuru Jumatatu alishtakiwa kwa kosa la kuharibu kipakatalishi akidai mpenziwe anakitumia kupokea jumbe za mapenzi kutoka kwa wanafunzi wa chuo Kikuu cha Egerton. 

Konstebo Wycliffe Gichuki alikanusha mashtaka hayo alipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Samuel Mungai na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh 50,000 na msimamizi mmoja wa kiasi kama hicho.

Mahakama ilielezwa kuwa mnamo Julai 13 katika mtaa wa Egerton wilayani Njoro, mshtakiwa alichukua kipatakalishi hicho na kukibwaga chini kwa nguvu.

Kifaa hicho chenye gharama ya Sh 40,000 mali yake Bi Jackline Wanjiru kilivunjikavunjika kisiweze kutumika tena.

Mahakama ilielezwa kuwa ubishi mkali ulizuka siku hiyo wakati Gichuki ambaye alikuwa amemtembelea mpenziwe aligundua jumbe 'moto moto’ kwenye kifaa hicho na akataka kujua ni kina nani hao wanadoea mpenziwe.

Walijibizana vikali huku Gichuki akitisha kumwadhibu vikali Wanjiru. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 4.