http://www.swahilihub.com/image/view/-/4177700/medRes/1803704/-/10e5arkz/-/waa.jpg

 

IEBC haikuwa tayari kwa uchaguzi Kenya - Muungano wa Ulaya

Marietje Schaake

Mwangalizi Mkuu wa Muungano wa waangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya (EUEOM) Bi Marietje Schaake ahutubu Agosti 10, 2017 katika hoteli ya Radisson Blu, Upper Hill, Kenya. Picha/EMMA NZIOKA 

Na WANDERI KAMAU

Imepakiwa - Wednesday, January 10  2018 at  19:59

Kwa Muhtasari

WAANGALIZI wa Uchaguzi wa Muungano wa Ulaya (EOM) Jumatano walilazimika kutoa ripoti yao mjini Brussles, Ubelgiji, wakidai kwamba serikali ya Kenya “haikuwa tayari kuwapokea.”

 

Bila kutoa ufafanuzi, mkuu wa ujumbe huo Bi Marietje Schaake, alisema kwamba walihisi kwamba serikali iliowaona kama “wakosoaji” wasiofaa, ndipo wakaamua kutoitoa nchini Kenya.

“Tualiamua kutoa ripoti yetu ughaibuni kwani mazingira ya Kenya hayakutufaa, hasa kutokana na taharuki ya kisiasa ambayo imeendelea kuwepo,” akasema Bi Schaake, kwenye mahojiano na 'Taifa Leo.’

Hata hivyo, kauli yao ilikosolewa vikali na Ubalozi wa Kenya nchini humo, ukitaja madai yao kama uongo, kwani haikufuata taratibu rasmi katika utoaji ripoti hiyo.

“Ni sikitiko kwamba (Bi Schaake) alitoa ripoti kuhusu hali ya uchaguzi wa Kenya mnamo 2017 bila kutufahamisha rasmi. Hakufahamisha asasi husika, wala kuzingatia mwafaka uliopo. Lengo lake ni kuharibia sifa serikali ya Kenya na watu wake,” akasema balozi wa Kenya nchini Ubelgiji Johnson Weru.

Kwenye ripoti hiyo, ujumbe huo ulikosoa mchakato wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8, ukisema kuwa asasi kuu, hasa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) hazikuwa tayari kuuendesha.

Ujumbe huo ulitoa ripoti yenye mapendekezo 29, yanayozilaumu asasi kuu kama IEBC, Idara ya Mahakama, Bunge la Kitaifa na vikosi vya usalama kwa kutotekeleza majukumu yake ifaavyo.

Ripoti iliilaumu IEBC kwa “kutokuwa huru” kwani ilionekana kuegemea katika baadhi ya mirengo ya kisiasa.

“IEBC inapaswa kuonyesha uhuru katika utendakazi wake, ili kujenga imani na uaminifu kutoka kwa umma,” akasema ripoti.

Kulingana na Bi Schaake, hilo ndilo lililopelekea mrengo wa Upinzani, NASA kutoshiriki katika Uchaguzi wa urais wa Oktoba 26.

Hasa, alitaja mauaji ya aliyekuwa Meneja Mkuu wa Teknolojia katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Chris Msando kama mfano bora ulioonyesha jinsi

Ripoti pia ilivilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kisai dhidi ya wafuasi wa NASA, ikiwalaumu polisi kwa kutumia risasi za chuma kuwakabili walipofanya maandamano.

Muungano wa NASA umedai kwamba karibu watu 215 wameuawa tangu Agosti 8 na polisi, hasa walipofanya maandamano.

Umedai kwamba polisi walikuwa wakiwalenga wafuasi wake, kwa kutumia visingizio kwamba walikuwa wahalifu.