Basi la Sauti Sol lahusika kwa ajali, dereva afariki

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Friday, April 21  2017 at  06:28

Kwa Mukhtasari

BASI la bendi ya Sauti Sol lilihusika kwenye ajali na kusababisha kifo cha dereva.

 

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Malindi lakini wakati wa mkasa huo wanamuziki hawa walikuwa ziarani nchini Nigeria baada ya kufanya shoo katika tamasha ya muziki ya Gidi Fest.

Basi hilo linasemekana kugonga lori lililokua limesimama na ambalo awali lilikuwa limehusika kwenye ajali na tuk tuk.

“Ajali iliyofanyika karibu na uwanja wa ndege wa Malindi ilisababisha watu wawili kujeruhiwa ambapo walipelekwa hospitalini na tunawaombea nafuu. 

Mioyo yetu inawaendeea familia na marafiki wa dereva wa basi lilioandikwa Live and Die in Afrika aliyefarki baada ya kuhusika kwenye ajali hiyo.

Hata hivyo hakuna mmoja kati yetu aliyehusika kwenye ajali hiyo,” waliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Basi hili hutumika hasa bendi hii ikiwa ziarani nchini ambapo limetolewa na mojawapo ya kampuni za usafiri nchini.