Bintiye Kibaki ajiunga na Deacons kama mkurugenzi

Na  BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  19:23

Kwa Muhtasari

Kampuni ya Deacons East Africa ilimteua Judith Kibaki kama mkurugenzi. Bi Kibaki atachukua wadhifa huo mara moja, baada ya kujiuzulu kwa Betty Mwangi kama mkurugenzi.

 

Deacons ilitangaza hayo mapema wiki hii.

Huenda Bi Kibaki akakabiliwa na changamoto kubwa ikizingatiwa kuwa hali ya biashara ni ngumu sana nchini.

Kampuni hiyo ilipata ongezeko la hasara la asilimia 244 katika muda wa miezi sita ya mwanzo ya 2017, hadi hasara ya Sh180 milioni, ikilinganishwa na nusu ya mwanzo wa 2016 ilipopata hasara ya Sh52 milioni.

Kulingana na usimamizi wa kampuni hiyo, hasara hiyo ilitokana na ukame, na udhibiti wa viwango vya riba kwa mikopo.