Fanyeni fujo muone, Uhuru aonya Wanajubilee

Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta akihutubu katika Ikulu ya Nairobi.. Picha/MAKTABA 

Na VALENTINE OBARA

Imepakiwa - Thursday, April 20  2017 at  13:40

Kwa Mukhtasari

RAIS Uhuru Kenyatta Alhamisi ametoa onyo kali kwa viongozi na wanachama wa Jubilee dhidi ya kuzua fujo kwenye mchujo utakaoanza Ijumaa hii.

 

Kwenye kikao na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta amesema polisi wamewekwa chonjo kupambana na yeyote atakayezua vurugu.

Alionya viongozi watakaoshiriki kwenye mchujo huo kwamba watakaosababisha ghasia watapokonywa nafasi ya kuendelea kushiriki katika michujo hiyo itakayofanyika sehemu tofauto nchini.

Rais pia ametaka maafisa watakaosimamia shughuli hiyo wahakikishe wanaifanya kwa njia ya haki na ya kuaminika.
"Watakaoenda kinyume na sheria watachukuliwa hatua kwa msingi wa kanuni za chama na pia kwa msingi wa sheria za taifa," akasema.

Zaidi ya hayo, amesema afisi yake iko wazi kwa wagombeaji ambao huenda wakataka kuelewana kuhusu mmoja kumwachia mwingine tikiti ya ugombeaji kabla mchujo uanze.

Amekana ripoti kwamba alimpigia debe Bw Peter Kenneth ambaye anapanga kupigania tikiti ya kugombea ugavana Nairobi dhidi ya Seneta wa Nairobi Mike Sonko.

Kulingana naye, viongozi wa chama na maafisa wakuu wa chama hawapendelei mgombeaji yeyote na wanataka wanachama wapate nafasi kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia.