http://www.swahilihub.com/image/view/-/3857644/medRes/1593906/-/yp9o59z/-/IMA.jpg

 

Hatimaye Imanyara arejea kwenye jukwaa la siasa

Gitobu Imanyara

Mbunge wa zamani wa Imenti ya Kati Bw Gitobu Imanyara (kati) alipoidhinishwa na wazee wa Njuri Ncheke nyumbani mwake katika kijiji cha Mariene Machi 20, 2017 kuwania kiti hicho. Picha/ KENNEDY KIMANTHI  

Na  KENNEDY KIMANTHI

Imepakiwa - Monday, March 20  2017 at  20:56

Kwa Mukhtasari

ALIYEKUWA mbunge wa Imenti ya Kati Bw Gitobu Imanyara sasa ametangaza kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kiti hicho tena kwa tikiti ya chama cha Maendeleo Chap Chap kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 8.

 

Wakili Imanyara aliyezungumza nyumbani mwake katika kijiji cha Mariene katika kaunti ya Meru alisema kwamba wakazi wengi wamemuuliza kuwania kiti hicho kutokana ubadhirifu wa kimaendeleo.

Bw Imanyara alisema baada ya mashauriano na wazee wa Njuri Ncheke ameamua kujiunga na chama hicho sifika.

“Hakina malumbano ya kisiasa kama vyama vingine hapa Meru,” Bw Imanyara alisema Jumatatu.

Mwanasiasa huyo aliyekuwa amestaafu kutoka siasa aliposhindwa na Bw Kiraitu Murungi katika kinyang’anyiro cha useneta wa Meru alisema atawatumikia wananchi inavyofaa.

Mbunge wa eneo hilo Bw Gideon Mwiti na katibu wa kaunti ya Meru Bw Julius Kimathi pia wametangaza kutawania kiti hicho.