Huawei kutoa mafunzo ya kidijitali Lavington

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  15:17

Kwa Muhtasari

Kampuni ya Huawei nchini imezindua kituo cha kutoa mafunzo ya kiufundi nchini.

 

Kituo hicho kimezinduliwa katika makao makuu ya Huawei, Lavington, na yanatarajiwa kutoa mafunzo ya hadhi ya juu kuhusiana na teknolojia ya kompyuta, mawasiliano ya simu na teknolojia za aina hiyo.

Kulinganga na Msimamizi wa Mafunzo Huawei eneo la Afrika Mashariki Bw Peter Thuo, wanafunzi watafunzwa kuhusiana na 4G, IoT, na teknolojia ya sasa ya mawasiliano ya kompyuta (cloud computing) na programu za kompyuta na majukumu ya mitandao ya mawasiliano.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwapa utaalamu zaidi wafanyikazi wake na washikadau kwa lengo la kuimarisha sekta ya habari, mawasiliano na teknolojia (ICT) nchini na mfumo wa dijitali.