http://www.swahilihub.com/image/view/-/2529704/medRes/881252/-/lp4ui5z/-/BDJUSTICEPAC2207A.jpg

 

IEBC kuwa na makamishna wapya wiki ijayo - Chepkonga

Samuel Chepkonga

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Haki na Sheria, Samuel Chepkonga katika kikao cha awali. Picha/DIANA NGILA  

Na CHARLES WASONGA

Imepakiwa - Wednesday, January 11  2017 at  17:50

Kwa Mukhtasari

Makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wataingia afisini wiki ijayo na kuanza kibarua cha kusimamia shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya.

 

MAKAMISHNA wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wataingia afisini wiki ijayo na kuanza kibarua cha kusimamia shughuli ya usajili wa wapiga kura wapya.

Shughuli hiyo itaanza Januari 15, 2017 hadi Februari 15, 2017 ambapo tume hiyo inalenga kusajili wapiga kura zaidi milioni sita (6 milioni).

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Sheria na Masuala ya Kikatiba (JLAC) Samuel Chepkonga Jumatano amesema kamati hiyo itaanza kazi ya kuandaa ripoti ya kamati yake kuhusu usajili wa watu saba waliopendekezwa kwa nafasi za mwenyekiti na makamishna wa IEBC.

"Tataanza kuandaa ripoti faafu ya Wakenya ambao tumewahoji jana (Jumanne) na leo (Jumatano). Tutawasilisha ripoti hiyo kwa kikao maalum cha bunge Jumanne wiki ujao. Tunaimani kuwa wapiga watapitisha ripoti yetu ambapo makamishna wapya wanatarajiwa kuanza kazi wiki hiyo," Bw Chepkonga aliwaambia wanahabari katika ukumbi wa County, Nairobi.

Hii ni baada ya Kamati yake kukabilia shughuli ya kuwahoji watu saba waliopendekezwa na Rais Uhuru Kenyatta kwa nyadhifa za Mwenyekiti na Makamishna wa tume hiyo.

Walihojiwa na Wakili Wafula Chebukati (nafasi ya mwenyekiti), Bi Consolata Nkatha Bucha Maina, Bw Boya Molu na Roseline Kwamboka Akombe ambao walipendekezwa kwa nyadhifa za makamishna.

Waliohojiwa Jumatano

Wengine waliohojiwa kwa nafasi za makamishna ni Dkt Paul Kurgat, Bi Margaret Wanjala Mwachanja na Profesa Abdi Guliye.

Saba hao watachukua nafasi ya tume ya zamani iliyoongozwa na Bw Ahmed Issack Hassan.

Chepkonga ambaye ni Mbunge wa Ainabkoi alisema kamati yake pia itawasilisha ripoti kuhusu ufaafu wa kiongozi mstaafu wa Kanisa la Kianglikana (ACK) Dkt Eliud Wabukala kwa wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

Akiidhinishwa, Askofu Wabukala atachukua nafasi ya Bw Philip Kinisu aliyejiuzulu mnamo Agosti 2016 kwa kuhusishwa na sakata ya Shirika la Vijana kwa Huduma za Taifa (NYS).