IEBC na Jubilee Party kujadili mchujo wa wawaniaji

Jubilee Party

Makao makuu ya Jubilee Party; jumba la Tuko Pamoja Towers eneo la Pangani Nairobi. Picha/JEFF ANGOTE 

Na CHARLES WASONGA

Imepakiwa - Friday, February 17  2017 at  14:26

Kwa Mukhtasari

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Jubilee Party wamebuni jopo la watu sita kujadili ikiwa tume hiyo itaendesha shughuli ya mchujo wa JP.

 

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Jubilee Party wamebuni jopo la watu sita kujadili ikiwa tume hiyo itaendesha shughuli ya mchujo wa JP.

Kila upande utatoa wawakilishi watatu.

Jopo hilo litafanya kikao cha kwanza Februari 28, 2017.

Mwenyekiti wa IEBC Bw Wafula Chebukati anasema kesi zilizowasilishwa kortini dhidi ya IEBC hazitaathiri mipango yake ya kuendesha uchaguzi Agosti 8, 2017.

"Zabuni nyingine ya ununuzi wa karatasi za uchaguzi itatangazwa wiki ijayo," amesema Chebukati.

Hii ni baada ya mahakama kufutilia mbali zabuni ya awali.

Anatoa hakikisho kuwa ununuzi huo utafanywa kwa wakati.

Mwenyekiti huyo anasema kuongezwa kwa muda wa usajili wa wapiga kura kutaigharimu IEBC Sh40 milioni kila siku.

Naye Mwaniaji wa Urais wa UDM Philip Murgor amelalamikia IEBC kwamba Rais na naibu wake wameanza kampeni za mapema ilhali zilifaa kuaza rasmi Juni 28.

Bw Chebukati amesema hakuna sheria inayobainisha siku ambayo kampeni za kisiasa zinafaa kuanza.