Jaji asimulia alivyomwokoa hakimu mfisadi

Na RICHARD MUNGUTI

Imepakiwa - Monday, October 3  2016 at  19:37

Kwa Muhtasari

JAJI wa Mahakama ya Rufaa Philomena Mbula Mwilu Jumatatu alisema alimwokoa hakimu mmoja wa mahakama ya Eldoret aliyekula mpenda mlungula.

 

Jaji Mwilu alisema alimkabili afisa mkuu wa polisi katika eneo la Eldoret (OCPD) na kumtaka ampe muda asuluhishe kisa hicho.

“OCPD alifika mahakamani kumtia nguvuni hakimu huyo. Nilimwita hakimu huyo katika afisi yangu na kumweleza akiri endapo alikuwa amechukua pesa za mlalamishi,” Jaji Mwilu aliambia jopo ya tume ya kuajiri wafanyakazi wa mahakama (JSC).

Aliongeza kusema , “Hakimu alikiri alikuwa amepokea mlungula kisha nikamshurutisha kuzirudisha mara moja.”

JSC iliambiwa na jaji huyo anayewania wa wadhifa wa DCJ kwamba alimshauri hakimu mwingine aliyekuwa mlevi wa kupindukia akabadilika na kugeuka kuwa mfanyakazi mwema na mwadilifu.

Jaji Mwilu alisema endapo atateuliwa kuwa DCJ atatumia mbinu mazugumzo kama mbinu ya kuimarisha utendakazi katika idara ya mahakama.