http://www.swahilihub.com/image/view/-/3111222/medRes/1276825/-/p41o8p/-/DNCOASTJOHO1003I.jpg

 

Joho aambiwa aache 'kebe na jeuri' zake kwa Rais

Hassan Joho

Gavana wa Mombasa Hassan Joho (kulia) azungumza na Kamanda mkuu wa polisi Pwani, Francis Wanjohi Machi 10, 2016. Picha/KEVIN ODIT 

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Sunday, January 8  2017 at  15:30

Kwa Mukhtasari

Mwa Kigumo Bw Jamleck Kamau na mwenzake wa Kandara Bi Alice Wahome wamemuonya gavana wa Mombasa Bw Ali Hassan Joho kuwa ajiandae kwa malimbikizi ya ukali wa serikali kufuatia mtindo wake wa kuikosea heshima.

 

MBUNGE wa Kigumo Bw Jamleck Kamau na mwenzake wa Kandara Bi Alice Wahome wamemuonya gavana wa Mombasa Bw Ali Hassan Joho kuwa ajiandae kwa malimbikizi ya ukali wa serikali kufuatia mtindo wake wa kuikosea heshima.

Walisema kuwa hatua ya Bw Joho ya kumzomea Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya umma Mombasa mwishoni mwa juma jana “ilikuwa ya kitoto,
kishenzi na ambayo haikustahili kamwe.”

Wakiongea katika eneo la Kamahuha wakati wa kuendeleza kampeni za Bw Kamau za kuwania ugavana wa Murang’a, Bw Kamau alimuonya Bw Joho kuwa “aambiwe na aliyeerevuka kuwa serikali sio ya rika yako na huwa na mbinu kali za kuandama yeyote anayeiona ikiwa haina makali.”

Huku cheche hizo za Bw Kamau na Bi Wahome zikitanda, Bw Joho akaondolewa walinzi wake sawia na mshirika wake mkuu kisiasa ambaye ni
gavana wa Kilifi Bw Amason Kingi.

Ni hivi majuzi tu ambapo Bw Joho aliagizwa arejeshe bunduki zake za kujilinda na inatazamiwa kuwa hil;a na njama zingine zitamwelekea kutoka kwa serikali, kwa mujibu wa Bw Kamau.

Alimtahadharisha Bw Joho kuwa “na bado usisahau kuwa kunao ndani ya serikali hii ya Rais Uhuru Kenyatta ambao ni wajanja kukuliko wewe na
wanaoweza wakawindana nawe kwa njia zote za kukudhihirishia kuwa serikali sio kibuyu cha mnazi.”

Alisema kuwa Bw Joho anachukulia Rais Kenyatta na serikali yake kama “isiyo na makali yoyote na ambayo inaweza ikaingizwa baridi na gavana
mmoja wa kipande kidogo cha taifa la Kenya.”

Akasema: “Bw Joho aambiwe na marafiki wake kuwa sisi tunaomuunga mkono Rais sio wajinga. Tuko na kila kitu ambacho kinamilikiwa na Bw Joho na
ambachjo kinampa joto la kuzua ujasiri wa kudharau Rais hadharani.”

Njia

Bi Wahome alimtaka Bw Joho aelewe kuwa “wewe uko na njia ndefu ya kutembea kisiasa kabla ya uafikie hadhi ya Rais Kenyatta. Ikiwa ni utajiri, Rais ni mkwasi kukushida. Ikiwa ni umaarufu, wewe umechaguliwa katika eneo moja tu la Kenya huku Rais akichaguliwa kitaifa. Ikiwa ni nguvu za mamlaka, rais anakurambisha sakafu kwa 9-0. Ulicho nacho kumzidi ni mdomo tu ulio na ulimi unaombingirika mdomoni kana kwamba umepata ajali ndani ya mdomo huo.”