Kampuni ya Ufaransa kuchora kituo kipya JKIA

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Thursday, January 11  2018 at  19:32

Kwa Muhtasari

KAMPUNI ya Ufaransa, Paris Aeroport imepata kandarasi ya kuchora kituo kipya cha abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi.

 

Kampuni hiyo ilipewa tenda hiyo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (KAA).

Kandarasi hiyo inajumuisha mchoro wa kituo hicho kipya pamoja na eneo la kuweka mizigo, alisema Gratien Maire, Mkurugenzi Mkuu wa ADP Ingenierie, inayomiliki Paris Aeroport.

Mradi huo unalenga upanuzi wa uwanja huo kwa upana wa mita 115,000 mraba, ikiwemo ni pamoja na majumba ya kuchukulia ndege, ilisema kampuni hiyo.

KAA inalenga kuongeza uwezo wa JKIA kutoka abiria milioni sita kila mwaka hadi milioni 10.3.

Mamlaka hiyo ilizindua vituo viwili vipya JKIA 2015.