http://www.swahilihub.com/image/view/-/4217178/medRes/1829265/-/dfy564z/-/LES.jpg

 

Kesi kuhusu shamba la Sh8 bilioni Karen kusikizwa Januari

Catherine Njeri

Bi Catherine Njeri akiwa nje ya Mahakama Kuu ya Milimani Jumanne, Nairobi baada ya kuahirishwa kwa kesi ya umiliki wa shamba la ekari 134 mtaa wa Karen, Nairobi. Picha/RICHARD MUNGUTI 

Na RICHARD MUNGUTI

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  15:38

Kwa Muhtasari

MAHAKAMA inayosikiza kesi za mashamba katika Mahakama Kuu ya Milimani Nairobi, Jumanne iliahirisha kesi ya umiliki wa shamba la ekari 134 katika mtaa wa Karen hadi Januari 12, 2018.

 

Mzozo wa shamba hili la thamani ya Sh8 bilioni ni kati ya aliyekuwa mjane wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Nairobi marehemu John Mburu , Carmelina Ngami na mwekezaji Horatius Dama Gama Rose.

Mahakama kuu iliombwa na wakili William Arusei imkubalie Bi Catherine Njeri anayesimamia mali ya Carmelina aliyefariki Septemba 2017 apate vyeti rasmi vya kumwezesha kufanya kesi hiyo.

Carmelina alikuwa amempa idhini Catherine kusimamia mali zake kwa vile alikuwa akiugua kwa muda mrefu.

Mahakama ilielezwa kuna ombi lililowasilishwa katika mahakama kuu inayoshughulikia kesi za masuala ya kijamii ndipo Catherine apewe vyeti vya kisheria kumwezesha kupambana na Da Gama Rose na mabwanyenye wengine.