http://www.swahilihub.com/image/view/-/3939798/medRes/1649469/-/o4w57h/-/TT.jpg

 

Kesi ya mauaji ya watoto 3 wa mwaniaji yaahirishwa

Kapsoya

Kutoka kushoto: Watoto watatu wa mwaniaji udiwani Kapsoya, Clifford Nyambane,6, Dan Nyamweya,5, na Glen Ongaki, 3 ambao waliuawa Mei 17, 2017. 

Na TITUS OMINDE

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  12:00

Kwa Muhtasari

KESI ya mauaji ya watoto watatu wa familia moja katika mtaa wa Kapsoya mjini Eldoret, ilihairiashwa katika mahakama ya Eldoret baada ya upande wa mashtaka ya umma kuomba muda zaidi kufanyia marekebisho mashtaka dhidi ya mshukiwa mkuu katika kesi hiyo. 

 

Upande wa mashtaka kupitia kwa mwakilishi wa kiongozi wa mashtaka ya umma Bw Zacary Omwenga, uliomba muda zaidi ili kufanyia mashtka husika marekebisho ili kujumuisha mashtaka ya mauaji dhidi ya mshukiwa mkuu Enoch Onsase ambaye ni ami ya watoto walioua kinyama. 

Omwenga alisema kuwa awali mshukiwa huyo katika mashtaka hayo alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya utekaji nyara. 

 Bw omwenga alisema kubadilsihwa kwa mashtaka hayo kulichochewa na kupatikana kwa miili ya watoto hao katika mto Nzoia wiki jana. 

Mshukiwa mkuu husika alipofikishwa kortin hakuruhusiwa kukana au kukubali mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Eldoret Charles Obulutsa. 

Hakimu Obulutsa alikubali ombi la upande wa mashtaka ambapo mshukiwa atarejeshwa mahakamani mnamo tarehe Juni 6, 2017. 

Kwa sasa, wachunguzi kutoka katika makao makuu ya idara ya jinai wamewasili mjini Elodret kushirikiana na wenzao katika kaunti ya Uasin Gishu kuendeleza uchunguzi huo. 

Mauaji ya watoto hao yamevutia hisia mbalimbali kutoka kwa viongozi wa matabaka mbalimbali ikizingatiwa kuwa baba ya watoto hao ni mgombezi wa kiti cha udiwani katika wadi ya Kapsoya kwa tiketi ya chama cha Kanu.