Kevin Lyttlei kutumbuiza wapenzi wa Dancehall nchini

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Friday, April 21  2017 at  06:25

Kwa Mukhtasari

Mashabiki wa muziki wa Dancehall nchini wana kila sababu ya kufurahia hasa ikizingatiwa kuwaa mwanamuziki maarufu wa mdundo huo kutoka Jamaica, Kevin Lyttle anatarajiwa kutumbuiza mashabiki nchini wikendi hii.

 

Mtunzi huyu anayefahamika kwa kibao chakeTurn me on anatarajiwa kutumbuiza mashabiki katika sherehe ya swanky Pool Party inayotarajiwa kuandaliwa katirka paa ya jumba la Diamond Plaza.

Mtumbuizaji huyu amepangiwa kuburudisha mashabki pamoja na wasanii wengine wa haiba ya juu kama vile Victoria Kimani, madijei Sexy Spin kutoka Nigeria, Purpl na Full Focus kutoka Amerika.

Msanii huyu atajumuisha watu wengine maarufu ambao watahudhuria hafla hiyo huku bei ya tikiti ikiwa Sh2000 kwa mabinti na Sh3000 kwa akina kaka.