Kirubi kununua kampuni ya Haco-Tiger East Africa

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  14:54

Kwa Muhtasari

Kampuni ya Haco-Tiger East Africa hivi karibuni itamilikiwa na Chris Kirubi. Mwekezaji huyo analenga kununua hisa zote za kampuni hiyo kufikia katikati mwa mwezi huu, kuwa mmiliki wa pekee wa kampuni hiyo.

 

Kampuni hiyo kwa sasa inamilikiwa na wawekezaji wawili, baada ya Haco na Tiger kuingia katika mkataba 2008.

Bw Kirubi 2008 aliuzia asilimia 51 ya kampuni ya Haco Tiger Brands, ya Afrika Kusini kwa zaidi ya Sh300 milioni.

Kutokana na tofauti zilizoibuka hivi majuzi kuhusiana na kuimarika kwa kampuni hiyo, Kirubi alipendekeza kununua hisa zote.

Mamlaka ya Kudhibiti Ushindani (CAK) tayari imekubalia Bw Kirubi kununua hisa hizo, huku Tiger Brands ikikubali kutoa sehemu yake ya umiliki kwa Haco-Tiger East Africa.