M-Kopa yaishtaki KRA ikitaka irudishiwe ushuru wa Sh35.7 milioni

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  18:52

Kwa Muhtasari

Shirika la ukopeshaji kwa njia ya simu, M-Kopa, limeishtaki KRA kwa kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kutotoza ushuru runinga za kidijitali zinazowashwa kwa kutumia nishati ya jua.

 

Shirika hilo linataka kurudishiwa Sh35.7 milioni lililotozwa na KRA kama ushuru. Lilishutumu shirika hilo la kukusanya ushuru nchini kwa kubatilisha uamuzi wake wa awali.

KRA haijajibu shtaka hilo, ila Jaji George Odunga amelitaka shirika hilo kufanya hivyo kabla ya kesi hiyo kusikilizwa Februari 7, 2018.

KRA katika uamuzi wa kibinafsi ilisema runinga hizo hazitatozwa ushuru zikiagizwa kutoka soko la kimataifa, lakini baada ya M-Kopa kuagiza, shirika hilo lilibatilisha uamuzi huo, na kusema kuwa runinga hizo zingetozwa ushuru, alieleza Pauline Githugu, Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa M-Kopa.