http://www.swahilihub.com/image/view/-/4076086/medRes/1740397/-/bj50yn/-/PA.jpg

 

Maduka yalazimishwa kuwapa wateja mifuko ya bure

Baadhi ya mifuko mipya inayotumiwa kupakia bidhaa baada ya mifuko ya plastiki kupigwa marufuku. PICHAA/ HISANI  

Na DENNIS LUBANGA

Imepakiwa - Thursday, December 7  2017 at  18:37

Kwa Mukhtasari

MADIWANI wa Uasin Gishu wamepitisha sheria itakayolazimisha maduka ya jumla katika kaunti hiyo kuwapa wateja wao mifuko ya kubebea bidhaa bila kuwalipisha.

 

Akiwasilisha mswada huo Jumatano, diwani maalumu Bi Catherine Barmao, alisema baada ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki miezi mitatu iliyopita, maduka ya jumla yamekuwa yakilazimisha wateja kununua mifuko ya kubebea bidhaa.

Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa umma kuhusu msimamo wa maduka ya jumla ambayo huwauzia mifuko kila mara wanaponunua bidhaa.

Huku akiunga mkono mswada huo, Diwani wa wadi ya Ng’enyilel, Bw David Sing’oei, alisema marufuku ya mifuko ya plastiki haifai kutumiwa na maduka kama sababu ya kupunja wateja.

“Mnakumbuka vyema kwamba mifuko ya plastiki ilikuwa ghali kabla ipigwe marufuku ilhali maduka yalikuwa yakitupatka bila malipo na hata ilikuwa ikichapisha majina yao kwenye mifuko hiyo. Sasa wahudumu madukani wanarundika tu kila kitu ndani ya mfuko mmoja,” akasema Bw Sing’oei.

Walikosoa hatua ya kulazimisha wateja kujinunulia mifuko.