Majumba 650 nchini ni hatari kuishi - Ripoti

Na  BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  19:12

Kwa Muhtasari

MAJUMBA kufikia 650 kote nchini sio salama kuishi. Ripoti hii ni kwa mujibu wa Bodi ya Kusimamia Majumba nchini (NBI).

 

Kulimngana na afisi hiyo, majumba hayo yanahitaji kubomolewa kwa lengo la kuwahakikishia usalama wananchi.

Hiyo ni ishara kwamba majumba hayo yamejengwa vibaya, au ujenzi wake umetekelezwa kwa kutumia malighafi isiyofaa au hazikujengwa kwa njia inayofaa.

Mtaa wa Huruma una majumba mengi zaidi ya aina hiyo(388) na kufuatwa na Thika Road(85) na Pipeline (65).

Mtaa wa Babandogo una majumba 38 yasiyo salama, Dagoretti (16), Umoja(18) na Nairobi West(9) na South B(5).

Kulingana na katibu wa NBI Bw Moses Nyakiongora, majumba hayo yanahitaji kubomolewa, “Tumetoa ushauri kwa serikali za kaunti kutoa ilani kwa wakazi kuhama,” alisema wakati wa kutolewa kwa ripoti kuhusiana na hali ya majumba nchini, Jumanne.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Nairobi, Kisii, Kitui na Athi River. Uchunguzi huo ulifanywa baada ya mikasa mingi kushuhudiwa maeneo mbali ikiwemo ni pamoja na Kisii na Nairobi.