Meneja wa benki akana wizi wa Sh15 milioni

Na RICHARD MUNGUTI

Imepakiwa - Thursday, September 28  2017 at  20:17

Kwa Muhtasari

MENEJA wa Benki ya NIC alishtakiwa Alhamisi kwa wizi wa Sh14.9milioni. Richard Moses Wambugu alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Kennedy Cheuiyot.

 

Alikanusha shtaka kwamba mnamo Septemba 23 aliibia mwajiri wake Sh14,999,850. Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Bi Everlyn Maika hakupinga ombi hilo akisema, “ni haki ya kikatiba kwa kila mshukiwa kuachiliwa kwa dhamana.”

Bw Cheruiyot alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh1milioni hadi Novemba 2, 2017.