http://www.swahilihub.com/image/view/-/4104190/medRes/1223807/-/10efky/-/BDLABOURDAY0105VV.jpg

 

Wamiliki matatu wamsihi Sonko asipunguze ada ya kuegesha magari ya kibinafsi

Mike Sonko

Gavana wa Nairobi Mike Sonko akihutubu awali. Picha/MAKTABA 

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Friday, February 1  2019 at  13:31

Kwa Muhtasari

Wamiliki wa matatu jijini Nairobi wamesema msongamano unaoshuhudiwa husababishwa na magari ya kibinafsi.

 

NAIROBI, Kenya

SERIKALI ya kitaifa kwa ushirikiano na ya kaunti ilikuwa imetangaza kuwa hakuna gari litakaloruhusiwa kuingia jijini Nairobi siku mbili kwa wiki, Jumatano na Jumamosi.

Agizo hilo lilipaswa kuanza Jumamosi ya kesho lakini Waziri wa Uchukuzi James Macharia mapema wiki hii alisema limeahirishwa kwa muda.

Kulingana na serikali ni kuwa pendekezo hilo la majaribio linapania kuondoa msongamano wa magari jijini Nairobi.

Wamiliki wa matatu jijini wamesema msongamano unaoshuhudiwa husababishwa na magari ya kibinafsi.

Kulingana na Jamal Mohamed, mwenyekiti wa muungano huo amesema changamoto za msongamano wa magari jijini Nairobi zitatuliwa iwapo magari ya kibinafsi yataondolewa katikati mwa jiji.

Kwenye kikao na waandishi wa habari mapema Ijumaa jijini Nairobi, Bw Jamal amemtaka Gavana Mike Sonko kufuta pendekezo lake la kushusha ada ya maegesho ya magari ya kibinafsi aliyotangaza kupunguza kutoka Sh300-200 mwezi Januari 2019.

"Magari ya kibinafsi ndiyo huleta msongamano wa magari Nairobi, ninamuomba ada ya magari hayo isalie ilivyokuwa awali," akasema.

Mwenyekiti huyo amesema punguzo hilo la ada litachochea magari ya kibinafsi kufurika jijini Nairobi.

Akifanya kampeni ya kuwania ugavana Nairobi 2017, Bw Sonko aliahidi wahudumu na wamiliki wa magari ya kibinafsi na matatu kwamba akichaguliwa atapunguza ada ya kuyaegesha.

Kabla ya serikali za ugatuzi kuanza 2013, magari yaliegeshwa jijini kwa hadi Sh100 kwa siku.

Hata hivyo, Gavana Evans Kidero ambaye aling'atuliwa na Sonko aliiongeza hadi kufikia Sh300.

Maegesho

Bw Jamal amemhimiza gavana kupunguza ada ya maegesho ya matatu, akihoji kando na kuzalishia serikali ya kaunti ya Nairobi pia imebuni nafasi za kazi kwa vijana.

Ada za matatu hutozwa tofauti kulingana na kiwango cha abiria inaobeba.