http://www.swahilihub.com/image/view/-/4035878/medRes/1714791/-/p6c1j0/-/desa.jpg

 

Uchukuzi wa shehena kupitia SGR kuanza Januari 2018

Atanas Maina

Mkurugenzi Mkuu wa KR Bw Atanas Maina. Picha/WANDERI KAMAU 

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  19:18

Kwa Muhtasari

SHIRIKA la Reli Nchini (KR) litaanzisha huduma ya uchukuzi wa bidhaa kwa kutumia reli ya kisasa (SGR), Januari mwaka 2018.

 

Kulingana na meneja mkurugenzi Atanas Maina, majaribio yamekuwa yakifanywa tangu Ijumaa kwa lengo la kulainisha ratiba ya uchukuzi.

Hatua hiyo ni kwa lengo la kuhakikisha kuwa ifikapo Januari, mfumo dhabiti upo, “Tunafanya majaribio ili Januari ikifika, mambo yatakuwa shwari,” alisema Bw Maina.

Kila kontena ya futi 20 italipishwa Sh50,000 na itachukua saa nane kwa mzigo kusafirishwa kutoka Mombasa hadi Naiorbi, aliongeza.

Huduma hiyo inatarajiwa kupunguza gharama ya uchukuzi wa shehena kutoka Mombasa hadi Nairobi, au kutoka Nairobi hadi bandarini Mombasa.

Magari manne yatakuwa yakifanya ziara za kila siku kati ya Mombasa na Nairobi, alisema Bw Maina.

SGR ilizinduliwa Mei mwaka huu na iligharimu Kenya Sh320 bilioni na ilitengenezwa kwa muda wa miaka tano.