http://www.swahilihub.com/image/view/-/3392916/medRes/1443413/-/3mc6b1/-/vifaru.jpg

 

Uingereza yatoa Sh2.1 bilioni kulinda wanyamapori Kenya

Vifaru

Vifaru wawili wakiwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Lewa. Picha/KENNEDY KIMANTHI 

Na BERNARDINE MUTANU

Imepakiwa - Wednesday, December 6  2017 at  15:21

Kwa Muhtasari

Kenya itanufaika baada ya serikali ya Uingereza kutoa Sh2.1 bilioni kupambana na mauaji haramu ya wanyamapori na biashara ya bidhaa zinazotokana na mauaji hayo.

 

Pesa hizo zimetolewa kufadhili mashirika yanayohusiana na Shirika la Umoja wa Mataifa yanayokabiliana na hali hiyo maeneo ya Afrika Mashariki na Afrika Kusini pamoja na Bahari Indi.

Serikali hiyo Jumanne ilitoa Sh2,094,438,668 kwa mashirika hayo kulenga “maeneo muhimu zaidi, maeneo ya mipakani na mbunga muhimu za wanyamapori.

Balozi wa Ulaya nchini Kenya Bw Stefano A. Dejak baada ya kutia sahihi mkataba huo alisema, “Mauaji haramu ya wanyamapori na uuzaji na ununuzi wa bidhaa zake ni biashara ya mabilioni ya fedha. Ili kukabiliana na suala hilo, tunahitaji kutafuta njia mpya za kushirikiana.”

Mkataba huo mpya unahusisha Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNDOC) Shirika la Kudhibiti Wanyama waliotishiwa na Shirika linalosimamia wanyama wa kuhamahama.

“Lengo kuu ni kuwalinda wa wanyamapori maeno ya mpakani kwa kushirikiana kutoa habari kuhusiana na hali katika maeneo hayo,” alisema Bw Dejak.