http://www.swahilihub.com/image/view/-/4609836/medRes/2007631/-/jk93ya/-/kapija2.jpg

 

Urithi Housing wafanya ubia na kituo cha uhamasisho wa Saratani

Urithi Housing

Wanachama wa Urithi Housing Co-Operative Ltd wakiwa katika hafla ya kufanya ubia na kituo cha Cancer Awareness Centre Of Kenya iliyofanyika Jumanne, Juni 12, 2018, katika Railways Club jijini Nairobi. Picha/LAWRENCE ONGARO 

Na LAWRENCE ONGARO

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  10:51

Kwa Muhtasari

Chama cha ushirika cha Uruthi Housing Co-operative Society Ltd kimefanya ubia na kituo cha Cancer Awareness Centre of Kenya, (CACK), kwa lengo la kuwapa heshima na kuonyesha upendo kwa wanaougua na Saratani.

 

NAIROBI, Kenya

CHAMA cha ushirika cha Uruthi Housing Co-operative Society Ltd kimefanya ubia na kituo cha Cancer Awareness Centre of Kenya, (CACK), kwa lengo la kuwapa heshima na kuonyesha upendo kwa wanaougua na Saratani.

Mkurugenzi wa kituo hicho cha CACK Bi Margaret Keige amewashukuru walioathirika kwa kuonyesha uvumilivu wakiugua maradhi hayo na kuwa na uwezo wa kukabiliana nayo kwa ukakamavu.

Amevipongeza vitengo vyote vya wasomi, serikali, na mashirika tofauti tofauti kwa kusaidia kukabiliana na maradhi hayo ambayo yamekuwa kero kubwa katika jamii.

Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kenya Railways jijini Nairobi ambapo iliwaleta pamoja washikadau wa serikali,  wasomi, na familia zilizokuwa na wapendwa wao walioathirika  kutokana na saratani.
Mgonjwa mmoja aliyepata saratani na kutibiwa akapata nafuu alipendekeza walioathirika wapewe matibabu  sawa katika hospitali zote nchini bila kubagua.
"Ni vyema  mgonjwa yeyote aliyeathirika  apewe matibabu sawa popote pale aendako kwa matibabu, mpango huo utawapa wagonjwa hao mwelekeo mwema usio na ubaguzi," alisema mmoja wa  waliopata nafuu baada ya kutibiwa Saratani.

Alisema wengi wa walioathirika na maradhi hayo husahaulika na baadaye ugonjwa huo huongezeka hadi kiwango hatari - awamu ya tatu.

"Hayo yote yanaweza kuzuiwa iwapo kutakuwa na hamasisho kwa wananchi popote walipo ili kujizuia," alieleza mwathiriwa huyo.

Kutuliza makali

Alisema inashangaza kuona ya kwamba wagonjwa wa Ukimwi hupewa dawa aina za ARVs, lakini walioathirika na Saratani hawapati dawa za dharura zinazoweza kutuliza makali.

"Jambo hilo ni muhimu sana na linastahili kuangaziwa haraka iwezekanavyo. Hatufai kuchukulia mambo kwa wepesi hivyo," alisema mwathiriwa huyo.

Mbunge wa Laikipia Mashariki, Bi Catherine Waruguru,  ambaye ndiye alikuwa mgeni wa heshima alikubaliana na mapendekezo yaliyonenwa huku akisema atafanya juhudi  kupeleka mswada bungeni ili kutangaza Saratani kama janga la kuangaziwa na kila mmoja.

Alisema atapendekeza serikali kutenga fedha zitakazosambazwa katika kaunti zote 47 ili zitumike kwa kutibu Saratani.

"Nitafanya kazi na kituo cha CACK, na wasomi pamoja na washikadau wote kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuhusu Saratani," alisema Bi Waruguru.

Mkurugezi wa mauzo wa chama cha Urithi Co-operative society, Bw Julius Macharia Gachanja, ameitaka serikali kuchukulia jambo hilo kwa uzito unaostahili ili kupambana vilivyo na Kansa.