Usasa Usasambu

Na WILLIAM HIMU

Imepakiwa - Thursday, June 7  2018 at  13:12

Kwa Muhtasari

  • Maudhui ya Usasa Usasambu yanagusia maeneo ambayo vijana wengi wanataka kujikita kama sehemu ya burudani
  • Soma ili ufahamu mengi kuhusu vijana hasa wa kike wanavyoathirika na utandawazi

 

SEHEMU YA PILI

(Kadri gari lilivyozidi kwenda ndivyo abiria walivyozidi kushuka na kupungua. Mwisho wakabaki Mwanakombo, Mwanaharusi na Mwanawima.)

Dereva: Mnaelekea wapi wasomi? (Anauliza huku akiwa anaangalia kwa kutumia kioo kilichopo mbele kabisa juu ya kiti chake.)

Mwanakombo:Stonetown (Anajibu kwa mkato.)

Konda: Hee! Mnakaa Stonetown mnasoma Chukwani? Si mnapata usumbufu sana!

Mwanawima: Ndio maisha yetu haya, huu mwaka wa tatu tunakimbizana na daladala.

Mwanakombo:  Matusi na kejeli za madereva na makondakta imekuwa sehemu ya maisha yetu, ndio maana hatuwashangai kwa maneno yenu ya  shombo na roho nyeusi kama zimekolezwa oili chafu. (Anaongea huku amebana pua) eti wa kusoma wametosha. (Anacheka kwa kejeli.)

Dereva: Oyaaa, ongea na wadogo zako vizuri mwana uwasaidie, hawajakula hao. (Anamkonyeza konda kwa siri na kupeana ishara za Dole gumba.)

Konda: Wagombanao ndio wapatanao, si unajua wanafunzi wakilegezewa wanajaa! Usawa huu tutaishije kwa vijisenti vya wanafunzi? Unakuta gari limejaa wanafunzi tu, ila msijali tuko pamoja.

Mwanakombo:  Tumeshawazoea bana! Hata wasipojaa mna kasumba ya kutowapenda wanafunzi kisa wanalipa nusu nauli.

Dereva: Hivyo hivyo, tuvumiliane warembo maana kwa upande wetu ukiwa mpole tu unaharibu kazi.

Mwanaharusi: Lakini kweli!

(Konda anakonyezana na dereva wake tena kisha anatoa simu yake ya mkononi na kumpa Mwanawima… bila kusema chochote.)

Mwanawima: Vipi? (Anamkodolea macho.)

Konda: Namba yako ya simu basi!

Mwanawima: Heee! Hiyo simu umeninunulia mpaka unataka namba yangu? Mimi sina simu. (Anafunga ushungi wake vizuri.)

Konda: Mmmm! Warembo kama ninyi mnakosaje simu? Yaani hata nokia ya tochi hamna?

Mwanawima: Hahaa, hatujaamua tu…

Konda: Ulimwengu huu tulionao mtu hatakiwi kukosa simu. Mnakosa mambo mengi mazuri. Usijali kesho kuna simu ipo nyumbani haina kazi   nitakupatia.

Dereva: Waambie watoto wazuri hakuna haja ya wao kuhangaika na usafiri tena, wameshakuwa rafiki zetu kila tukipita wakiliona gari letu wapande free.

Mwanakombo: Hapo mtakuwa mmetusaidia sana maana saa ya kurudi tunapata shida haswaa! Tukipata hiyo simu tutakuwa tunawajulisha tulipo.

Konda: Sawa, kesho saa kumi na mbili tutakuwa tumeshafika kituoni, mjitahidi kuwahi.

Mwanawima: Hahaa! Ila usumbufu hatutaki.

Konda: Hamna usumbufu bwana, kwani nyie watoto?

Dereva: (Anamwangalia Mwanaharusi huku akiwa anaendelea  kuendesha gari) Mbona huyu mwingine haongei?

Mwanakombo: Huyo anaongea kama chiriku, haujamzoea tu.

Mwanaharusi: Mimi simo kwenye mambo yenu, (Anamwambia kwa sauti ya chini…)

Konda: Hakuna shida, hata peponi hawaingii watu wote...

Mwanawima: Huyo ndio kawaida yake ila anaongea sana tu. Inabidi   

umzoee tu.

Mwanaharusi: Mmmh! (Anaguna na kuendelea kuangalia nje. DirishaniMaongezi yanazidi kunoga, taratibu wanafika Stonetown wanashuka, wanaagana na konda na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Njiani maongezi yanaendelea.)

Mwanaharusi: Heeee! Yaani hata hamuogopi? Hiyo simu ukipewa utakuwa unaiweka wapi?

Mwanawima: Tutatumia wote, siku nyingine nakaa nayo mimi na siku nyingine unakaa nayo wewe.

Mwanaharusi: Weee! Weeeee! Enheeee! Mama yangu ananifuatilia sana, pia sina shida na simu kwa sasa!

Mwanawima: Heheee, haloo! Ama kweli aliyelala usimuamshe… (Mwanakombona Mwanawima wanacheka.)

Mwanakombo: Hakiharibiki kitu, kama hutaitumia tutaitumia mimi na Mwanawima. Mambo ya wasapu, twita, fesibuku kwa sana. Aiiii, tena navopenda miziki sitapata shida ya kuchungulia kwenye televisheni na kuvizia vipindi vya muziki.

Mwanawima: Mimi napenda sana instagramu, kesho tukiipata tu tukajiunge tuwe tunaangalia picha. Achana na huyo asiyejua wapi ulimwengu unakotoka na wapi unakokwenda.

(Mwanakombo anafika nyumbani kwao jua limeshazama anamkuta baba yake amekaa sebuleni ameshikilia ‘remote’ ya runinga yake, anamsalimia na kupitiliza chumbani kwake.)

Mwinyiheri: Mtumwa njoo. (Anamuita dada wa kazi.)

Mtumwa: Abee baba, nakuja… (Anaenda kwa baba yake mbiombio.)

Mwinyiheri: Leo umepika nini? Halafu umekumbuka kuniandalia ile

juisi yangu?

Mtumwa: Leo nimepika wali kwa samaki, pia juisi yako ipo tayari.

Mwinyikheri: Basi vizuri.

(Mtumwa anaanza kutenga chakula mezani huku Mwanakombo akiwa chumbani mwake.)

Mwanahawa: (Anafungua mlango) Wewe Mwanakombo, huko chumbani una kazi gani? Nishakwambia ukirudi nyumbani uwe unamsaidia dada yako kufanya kazi za humu ndani.

Mwanakombo: Mamaaaa! Mimi pia nachoka.

Mwaahawa: Umechoka na nini wewe? Mwenzako kapika na bado akutengee chakula?

Mwanakombo: Kusoma pia kunachosha mama.                 

Mwanahawa: Shika adabu yako! Sasa kama umechoka nani akutengee