http://www.swahilihub.com/image/view/-/3889706/medRes/1615014/-/e09p9m/-/AY.jpg

 

Wacheshi kukusanyika kumzika Ayeiya

Ayieya

MVUNJA mbavu wa kipindi cha Churchill Show kwenye runinga ya NTV Emmanuel Makori almaarufu Ayeiya akiwa jukwaani awali. PICHA/ HISANI 

Na  PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Friday, April 21  2017 at  06:20

Kwa Mukhtasari

Siku chache baada ya kifo chake, jamaa, marafiki na mashabiki wa mcheshi Emmanuel Makori al-maarufu Ayeiya, walikusanyika hapo siku ya Jumatano Aprili 19, 2017 kwa ibada ya wafu katika Kanisa la Pentecostal Church, Karen jijini Nairobi.

 

Miongoni mwa waliohudhuria na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwenda zake ni pamoja na pamoja na wacheshi Daniel Ndambuki al-maarufu Churchill, Fred Omondi, Consumator, YY na Chipukeezy miongoni mwa wenginne.  

Ayeiya alifariki Ijumaa iliyopita baada ya gari alimokuwamo kugonga mlingoti wa umeme katika eneo la Karen.

Ayeiya anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Aprili 21, 2017 katika eneo la Nyansiongo, Kaunti ya Nyamira.