http://www.swahilihub.com/image/view/-/2788044/medRes/1061304/-/a0s7taz/-/DNEldPokot0910a.jpg

 

Gavana Lonyangapuo ashauri wakulima kununua mbegu bora

Seneta wa Pokot Magharibi Prof John Lonyangapuo

GAVANA wa Pokot Magharibi Prof John Lonyangapuo. Picha/JARED NYATAYA 

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, March 13  2018 at  11:53

Kwa Muhtasari

Idara ya utabiri wa hali ya anga mapema wiki hii imetangaza kwamba taifa litapokea mvua kubwa kwa siku nne zijazo mtawalia.

 

IDARA ya utabiri wa hali ya anga mapema wiki hii imetangaza kwamba taifa litapokea mvua kubwa kwa siku nne zijazo mtawalia.

Pia, ilieleza kuwa mvua itaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo hadi Mei 2018.

Katika kaunti ya Pokot, Gavana John Lonyangapuo akihutubu Jumanne ameshauri wakazi wake kuchagua mbegu bora za nafaka msimu wa upanzi ukiwa tayari umebisha hodi.

"Kuna haja ya kutilia mkazo wakulima wapande mbegu bora, zenye mazao tele," ameshauri Gavana Lonyangapuo akihutubu Pokot Magharibi.

Gavana huyo amefichua kuwa serikali yake inafadhili wakulima wasiojiweza mbegu za upanzi, ikiwa ni pamoja mbolea ya kisasa.

"Tumelenga kati ya wakulima 300-400, kando na kuwapa mbegu pia tunawafadhili mfuko mmoja wa mbolea," ameeleza.

Gavana Lonyangapuo alikuwa ameandamana na wataalamu wa mchanga, ambapo pia ameeleza haja ya kutambua uhalisia wa mchanga na mimea inayofaa kukuzwa.

Kiangazi kilishuhudiwa mapema mwaka 2018 na mvua ilipoanza kunyesha Machi serikali kwa ushirikiano na washikadau husika katika sekta ya kilimo iliwashauri wananchi kupanda miche ya miti ili kuhifadhi vyanzo na chemichemi za maji.

Kutokana na mvua inayoshuhudiwa, wakulima nchini wako katika harakati za upanzi.

Kaunti za Trans-Nzoia na Uasin-Gishu ni baadhi ya zinazofanya kilimo cha nafaka hasa mahindi na ngano kwa wingi.

Wakenya hutegemea mahindi kuwafadhili unga wa mahindi, na ngano wa chapati na mahamri.