Mzee mwenye umri wa miaka 60 ashtakiwa kumnajisi mtoto wa jirani

Na BRIAN OCHARO

Imepakiwa - Friday, January 11  2019 at  13:00

Kwa Muhtasari

Mzee mwenye umri wa miaka 60 ameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa akikabiliwa na kosa la kumnajisi mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka mitano.

 

MOMBASA, Kenya

MZEE mwenye umri wa miaka 60 ameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa akikabiliwa na kosa la kumnajisi mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka mitano.

Rajab Mohamed anashtakiwa kwa kuchafua mtoto huyo katika eneo la Baghaan kwenye kaunti ndogo ya Likoni huko Mombasa.

Karatasi ya mashtaka inasema mshukiwa kimaksudi na kinyume na sheria alichafua mtoto huyo kwa nyumba yake.

Mahakama iliambiwa mamake mwathiriwa alikuwa ameenda sokoni wakati mzee huyo alichafua mtoto wake.

Mzee huyo ambaye alionekana kuwa na wasiwasi wakati wa kusomewa mashtaka alijikakamua kujitetea dhidi ya mashtaka hayo.

“Si kweli kwamba nilichafua mlalamishi, mashtaka hayo ni ya uongo,” alisema

Bw Mohamed alikabiliwa na shtak la badala ya kufanya kitendo kisicho cha madili na mtoto mdogo.

Kupapasa sehemu za siri

Mzee huyo anashtakiwa kupapasa sehemu za siri za mtoto huyo kwa kutumia uume wake.

Mshukiwa huyo alikanusha mashtaka hayo ambayo anahutumiwa kufanya mnamo Desemba 4, 2018, alipofikishwa mbele ya Hakimu Mkaazi Christine Ogweno.

Mshukiwa huyo aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.

Kesi hiyo itatajwe tena Januari 28 ili kutolewa mwelekeo zaidi.